Header Ads Widget

MBUNGE MATHAYO AENDELEA KUWEZESHA VIJANA MKOPO NAFUU WA PIKIPIKI

 

Na Shomari Binda-Matukio Daima-Musoma 

MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea kuwezesha vijana mkopo nafuu wa pikipiki.

Jana aprili 22,2025 vijana 75 wameingia kwenye utaratibu huo na kupata pikipiki ambazo watarejesha kwa kipindi cha miezi 11 na kuweza kumuliki.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo ambunge huyo amesema lengo lake ni kusaidia vijana waweze kumiliki pikipiki zao na kuiiinua kiuchumi.

Amesema amekubaliana na moja ya kampuni zinazouza pikipiki na kijana anayetoa kiasi cha shilingi laki 3 anamuongezea laki 1 na elfu 9 na kuendelea kulipa kidogo kidogo.


Mathayo amesema mkopo huo ni nafuu tofauti na mikopo mingine ya gharama kubwa na inayolipwa kwa muda mrefu ambayo itawasaidia vijana.


Mbunge huyo amesema hii ni awamu ya pili ya vijana kuwezeshwa kwenye upande wa pikipiki na kudai kuendelea na utaratibu huo kila vijana watapojitokeza.


" Hii ni awamu ya pili tunawapatia vijana pikipiki za mkopo nafuu ili baadae waweze kuzimiliki na kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.


" Zoezi hili ni endelevu na tutaendelea kuwawezesha vijana wamiliki fedha mfukoni ili maisha yaweze kuendelea",amesema.


Mwenyekiti wa chama cha bodaboda manispaa ya Musoma Stephine Silasi amemshukuru mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwawezesha vijana kiuchumi.


Amesema vijana waliochukua mkopo nafuu wa awali wanaendelea vizuri na kuamini waliopata awamu hii nao wataendelea vyema na shughuli zao.


Baadhi ya vijana waliowezeshwa kupata pikipiki wamesema watazitunza vizuri na kurejesha ili baadae waweze kumiliki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI