.
Askofu Mkuu wa kanisa la Africa inland church Tanzania AICT Mussa Magwesela
NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA
Askofu Mkuu wa kanisa la Africa lnland Church Tanzania (AICT) Mussa Magwesela amewataka waimbaji wa kaya ya AIC Chang’ombe Choir (CVC) kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutunza chapa ya uimbaji bila kuichafua wala kuitumia vibaya Kwa tabia zozote zile Kwa mtu moja moja.
Akizungumza Katika kongamano la jumatatu ya pasaka liloandaliwa na kwaya hiyo lililofanyika Jijini Mwanza lenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao wanaifahamu( CVC) na kuwafahamisha mipango waliyonayo pamoja na mafanikio waliyoyapata.
Magwesela ameeleza kuwa ni rahisi kuchafuliwa na kuichafua chapa walionayo waimbaji hao kutokana na tabia ya mtu moja moja aliyonayo inaweza kuwa ni ulevi, uvutaji wa sigara, usherati, na kuona yupo sehemu ya siri ambayo hawezi kujulikana.
"Mnapaswa kuangalia namna ya kuilinda chapa hiyo mliyonayo ili ikitokea mtu yeyote anakwenda sehemu nyingine kuwawakilisha anakuwa balozi mzuri kupitia kwaya yenu" Alisema Magwesela.
Aidha Kwa upande mwingine amewataka waimbaji hao kuwa wabunifu Kuongeza umahili katika uimbaji ili kusudio la uimbaji liwe la viwango vya juu sana ili kusudio la Mungu liweze kutumia kupitia uimbaji wao.
"katika Kuendelea kumtumikia Mungu ni lazima kuwa jasiri katika huduma ya uimbaji na kuwa mbunifu Kwa kile mnachokifanya Mungu hakutuumba sisi kuwa kama roboti au mashine alitupatia akili ili tuweze kujiongeza" Alisema Magwesela.
Katibu Msaidizi wa kwaya ya AIC Chang’ombe Choir (CVC) Joel Erasto ameeleza kuwa kutokana na uimbaji huo wamekuwa kuwashirikisha na kuwaleta vijana pamoja katika makundi ya kidini ili kuwasaidia kuwa na nuru ya kuendelea kuwalea na kuwaweka katika mazingira rafiki ili wasiendelee kuishi maisha ya uovu.
"Kuna maisha ambayo vijana wanaweza kuyapitia huko nje kaba ya kumjua Mungu kama uvutaji wa bangi, sigara, na unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza kusababisha jamii ya kitanzania isiweze kunufaika na kundi hilo" Alisema Erasto.
0 Comments