Header Ads Widget

MAWAKILI WA SERIKALI KUKUTANA DODOMA KUJADILI MASUALA YA KITAALUMA

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima APP Dodoma

NAIBU Waziri Mkuu, Doto Biteko, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali (GLO) unaotarajiwa kufanyika Aprili 14 na 15, 2025 jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 12, 2025, Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, AmeDeus Shayo, amesema mkutano huo utatoa jukwaa kwa mawakili hao kujadiliana masuala mbalimbali ya kitaaluma pamoja na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mkutano huu ni fursa mahsusi kwa wanachama wetu ambao ni mawakili na wanasheria kutoka taasisi mbalimbali za umma, kujengeana uwezo, kubadilishana uzoefu na kuimarisha maadili katika utumishi wa umma,” amesema Shayo.

Mbali na Naibu Waziri Mkuu, wageni wengine mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais huyo amesema mkutano huo pia ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alilolitoa wakati wa uzinduzi wa chama hicho mnamo Septemba 22, 2022.

“Nitoe rai kwa waajiri wote kuwawezesha mawakili na wanasheria wao kushiriki kikamilifu katika mkutano huu muhimu kwa sababu unahusiana moja kwa moja na masuala ya kitaaluma na maendeleo ya sekta ya sheria nchini,” amesema Shayo.

Ameongeza kuwa zaidi ya wanachama 2,000 wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo ambao pia utakuwa jukwaa la kufanya tathmini na kuweka mwelekeo mpya katika kuimarisha mchango wa mawakili wa serikali kama walinzi wa uchumi wa taifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI