Sehemu ya kwanza.
Jimbo la Nzega Mjini linaongozwa na Mbunge Hussein Mohammed Bashe tangu mwaka 2015 baada ya kugawanywa kwa jimbo la Nzega na kuwa na majimbo mawili, yaani jimbo la Nzega Mjini na jimbo la Nzega Vijijini.
Kuna mambo lukuki ambayo bwana Hussein Bashe aliyaahidi wakati wa uchaguzi wa 2015 na 2020, lakini nitataja machache aliyoyaahidi na mengine nje ya ahadi hizo ambayo aliyafanya kabla na aliyokuja kuyafanya katika jamii baada ya kuwa Mbuge.
Kabla ya yote nitangulie kusema kwamba, tunafanya makosa kama jamii na wala hakuna jambo la kushangaza katika kutenda makosa.
Kila mtu hufanya makosa maishani mwake na kila jamii pia. Ni jambo la kawaida.
Jambo ambalo si la kawaida ni pale mtu mwenye akili timamu anapofanya kosa na asijue kwamba kafanya kosa, ama akafanya kosa na akajua kwamba kafanya kosa na kisha akajisahau na kuja kulifanya kosa lile lile.
Jamii zenye kujali maendeleo hujifunza kutokana na makosa zilizoyatenda huko nyuma ili zisiyarudie.
Jamii zisizojali maendeleo huishi kwa kuangalia kilichopo mezani leo na zisijali kilichotendeka jana wala juzi.
Jamii za aina hii zinaweza zikawa zinarudia makosa yale yale kila siku na kila mwaka hasa katika miaka ya uchaguzi ikawa ndiyo hulka ya jamii hizo. Jamii ya aina hii bila shaka tunaishuhudia hapa kwetu Nzega, inasikitisha sana kuona wapiga kura wakiwachagua wanasiasa wale wale ambao wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya jamii.
Ili kukumbuka ni mahali gani zilikosea katika historia yake, jamii za kale ziliweka simulizi, hadithi na ngano ili kuwafundisha vijana wake mambo yaliyotendeka zama za kale kama mafundisho kwa watoto na vijana.
Siku hizi mambo kama hayo yanawekwa kwenye vitabu. Laiti kama tungekuwa tunayafundisha kwenye makongamano na mikusanyiko mingine ya kijamii na hata kuyaandika kwenye magazeti au mitandao ya kijamii mambo tunayoyafanya, mazuri na mabaya, tungekuwa tumejijengea hazina ya ujuzi na maarifa katika mambo mengi ya msingi.
Kwa bahati mbaya jamii kama ya Nzega, inaonekana haina hazina hiyo kwa sababu haiyumuniki mambo yanayofanyika na kuendelea kufanyika katika jamii siku hadi siku na hatuna kumbukumbu ya mambo tuyatendayo.
Fikiria juu ya chaguzi mbalimbali za wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji, uchaguzi wa madiwani na wabunge, unapofanyika uchaguzi iwe ni ndani ya chama na ule wa dola, wapiga kura huwa hawazingatii sifa za wagombea, matokeo yake baada ya uchaguzi wanaanza kulalamikia uongozi ule ule waliouweka madarakani wao kwa mikono yao wenyewe.
Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 na ule wa mwaka 2015, bwana Hussein Bashe aliwaaminisha wananchi na wapiga kura kuwa ni mtu mwenye haiba nzuri na mwenye taswira inayonesha kuwa ataweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kimaendeleo hasa ya jamii.
Msingi wa ushawishi wake aliujenga katika kutoa pesa kwenye mihadhara au mikusanyiko ya kijamii kama misiba na sherehe mbalimbali.
Fedha hizo zinaaminika kuwa alizilitoa kwa Edward Lowassa na Lostam kwa lengo la kumng'oa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Nzega, Mzee Lucas Selelii na pia awasaidie katika biashara zao.
Mwaka huo wa 2010 bwana Hussein Bashe hakufanikiwa kurudishwa jina lake kutikana na sababu mbalimbali za rushwa na kwamba hakuwa raia wa Tanzania, likarudi jina la Dk. Hamis Kigwangalla na kuwa Mbunge wa jimbo la Nzega.
Kilichotokea ni kwamba, bwana Hussein Bashe alianza kumhujumu Mbunge Dk. Kigwangalla, ama kwa makusudi au kwa kutojua kwamba hujuma zile zilikuwa ni za kuwahujumu wananchi wa Nzega na sio Dk. Kigwangalla.
Baada ya uchaguzi ule wa 2010, Dk. Kigwangala alianzisha harakati za kupigania kudai Bilioni 10 ambazo ni fidia ya ushuru wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kutoka katika Mgodi wa Resolut Nzega.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Mzee Mbozu aliunda Tume iliyoongozwa na Mbunge Dk. Kigwangalla na wajumbe ambao ni Diwani wa Itilo Furaha Bazilio, Diwani wa Uchama Mzee Kaloli, Diwani wa Nzega ndogo Nasra, Diwani wa Sigili, Pele, ambao ndiyo waliosafiri kwenda makao makuu Dodoma ili kukutana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stivin Masele.
Jitihada hizo zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia hadi Wakurugenzi wa Kampuni ya Risolut kukubali kulipa hizo pesa zote japo kwa awamu, awamu ya kwanza Resolut walilipa Bilioni 2.4, na mipango mizuri ikaanza kufanyika juu ya matumizi ya hizo pesa.
Kwanza Baraza la Madiwani ilibidi kupeleka wataalamu mkoani Mbeya kupata mbinu na uzoefu wa kibenk juu ya kuanzishwa kwa saccos ili kuja kufanya hivyo Wilayani Nzega, na zingine zilitengwa kwa ajili ya kununua mitambo ya kuchimba visima vya maji na kutengeneza barabara.
Sasa kwa sababu ya ufinyu wa akili na uhaba wa fikra pevu za kimaendeleo, bwana Hussein Bashe badala ya kushukuru na kuunga mkono maendeleo ya wananchi wa Nzega, yeye akili yake ilibaini kabisa kuwa hatakuwa na hoja za kuwaeleza wananchi uchaguzi unaofuatia, akawalaghai na kuwashawishi
madiwani kwa nguvu ya pesa na kuwatishia kuwa hawatarudi uchaguzi uliokuwa ukifuata ili wakakatae malengo ya msingi na kubadilisha maazimio ya Baraza lao la Madiwani, kuanzia hapo Baraza la Madiwani likagawanyika vipande viwili.
Kundi kubwa la Madiwani likakubaliana na fikra finyu za Hussein Bashe za kukwamisha maendeleo kwa kutonunua mitambo hiyo na badala yake fedha zile zigawanwe na kwenda kujenga maabara kila kata, ambapo matokeo yake zilifisadiwa na kuliwa.
Kwa mtu au mwanasiasa mwenye nia njema na watu wake hawezi kukwamisha maendeleo ya wananchi yanayofanywa na uongozi uliopo madarakani, badala yake kama anataka kushindana katika siasa atakuwa na mbinu mbadala au mpya za kuboresha zaidi au kuja na mambo mapya kabisa ya kuitoa jamii ilipo kwenda mbele.
Kutokana na ukweli huo, kuwa Hussein Bashe ni mtu asiye na maono ya kimaendeleo ya wananchi, wala nia njema kwa wananchi, zaidi ya kujinufaisha binafsi, mambo kadhaa aliyafanya kwa Madiwani ambao hawakuwa tayari kutumika ili kuwahujumu wananchi; madiwani hao ni pamoja na Nasra, Bazilio, Mzee Kaloli, Mzee Sawaka, Mzee Nchimani na Zaituni Diwani wa viti maalumu, hawa wote walishughulikiwa ili wasirudi uchaguzi wa mwaka 2015.
Hili halijaishia hapo, pia na ye yote aliyeonyesha kutokubaliana na mambo ya Hussein Bashe alimshughulikia kwa namna moja au nyingine, iwe ni katika biashara, au katika siasa na maisha yake binafasi.
Tunao wengi ambao wameumizwa na huyu bwana Hussein Bashe, Shabuti mpaka leo hana hamu kwa jinsi alivyomfanyia, sijui ni nini au hila za maendeleo, Shabuti alimfadhili Hussein Bashe milioni 70 katika uchaguzi - lakini Hussein Bashe akaja kumlipa ubaya kwa kumchongea kwa waziri wa mazingira ili afungiwe miradi yake.
Halikadhalika Mfanyabiashara Mashili, huyu naye amemfanyia hila na fitina kiasi kwamba miradi yake mingi alifungiwa, mingine akaamua kuihamisha na kuipeleka mikoa mingine, kisa ni kwamba anatumia haki yake ya msingi kuomba kuwawakilisha wananchi wake kupitia jimbo la Nzega Mjini.
Hayo ni moja tu ya mambo ya hovyo anayoyafanya bwana Hussein Bashe na ambayo wapiga kura wengi wanayajua, lakini wametishwa na hawana la kufanya zaidi ya kufuata maelekezo ya bwana Hussein Bashe na genge lake.
Tukutane makala ijayo sehemu ya pili.
Kwiyeya Singu. 0784977072
0 Comments