Na Matukio Daima Media-Musoma
TIMU ya soka ya CRDB benki tawi la Musoma kesho aprili 26,2025 katika kusherehekea sikukuu ya Muungano itashiriki bonanza la Muungano kwa kucheza na FFU Mara.
Mchezo mwingine wa bonanza hilo utazikutanisha timu ya Musoma Veteran dhidi ya Biashara United Veteran na washindi wa michezo hiyo watakutana kwenye fainali.
Mratibu wa bonanza hilo Shomari Binda amesema maandalizi yote kuelekea bonanza hilo yamekamilika na kinachodubiliwa ni muda.
Amesema lengo la bonanza hilo ni kusherehekea pamoja sherehe za Muungano na kujenga mahusiano..
Binda amesema bonanza hilo limekuwa likifanyika kila mwaka ili kuwa pamoja kwa wadau kukutana na kushiriki michezo.
Amesema mshindi wa bonanza hilo ataondoka na zawadi ya mbuzi na kila timu shiriki itapata cheti cha ushiriki wake
0 Comments