Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Steven Wasira amesema kuwa Chama hicho kinaanda Ilani nzuri ya Uchaguzi 2025-2030 kwa kuanzisha Vituo vya Matrekta yatakayowalimia kwa bei nafuu wananchi ili wajikwamue kiuchumi.
Aidha Wasira, amewataka Wananchi kuendelea kuunga Mkono Chama hicho ambacho kinaunga mkono Tanzania ya Amani.
Makamu huyo ameyasema hayo leo kwa nyakati tofauti kwenye Mkutano wa ndani wilaya ya Meatu pamoja na Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nkoma wilayani Itilima.
Wasira amesema kuwa katika Ilani inayokuja, lazima waongeze uzalishaji wa Umeme kwani kuna kazi kubwa iliyofanyika ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Samia ikiwemo kufanya mabadiliko ya Kidemokrasia na kulinda amani.
"Maendeleo hayana mwisho, baada ya Uchaguzi tutaanzisha vituo vya Matrekta ili walime kisasa na kwa bei nafuu ili wakulima wajikwamue kiuchumi...Upinzani hawana kazi zaidi ya kuchochea na kufanya maandamano, hawana jipya, hawana sera mpya, sisi tunashughulika na Maendeleo, Afya, Uchumi wao hawana mbadala." Amesema.
Ameongeza kuwa tangu CCM iliporithi mikoba ya TANU na Afro Shiraz imeendelea kusisimamia Maendeleo ya watu kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji , Umeme, na Barabara.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amesema Ilani ya CCM imewaelekeza kujenga Zahanati, vituo vya Afya, na hospitali jambo ambalo wameshakamilisha.
"Rais Dk. Samia na mtangulizi wake walisema wataijenga Itilima, awali ilikuwa na shule 92 leo kuna shule 102...tuliahidi kujenga zahanati, awali tulikuwa na Zahanati 36 leo ziko 45, suala la Maji, Itilima ilikuwa imeshindikana tumepata shilingi Bil. 12 na Maji yapo Itilima." Amesema Njalu.
Mwisho.
0 Comments