Header Ads Widget

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBEGU ZINAZO KABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Na Matukio Daima Media ,Arusha

Wakulima wa mazao mbalimbali ikiwepo mbogamboga na matunda nchini, wametakiwa kutumia mbegu bora  zinazoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi .

Hivi sasa Ongezeko la joto ardhini katika maeneo mengi nchini linalosababisha  mbegu za mazao na mazao yaliyopandwa kuharibika na kushindwa kutoa mazao bora.


Mtaalam wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania, Chonya Wema akizungumza katika siku ya wakulima ya maonesho ya mbegu jijini Arusha, ambayo huandaliwa kila mwaka na kampuni hiyo, alisema kampuni hiyo imeanza kuzalisha mbege zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 Wema aliwataka wakulima kutumia mbegu  hizo kwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa mimea ili kunufaika na kilimo na kuongeza uzalishaji.

Alisema kuwa hivi sasa kuna aina nyingi ya mbegu lakini baadhi ya hizo mbegu haziwezi kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa na kupelekea kushambuliwa na wadudu wa mimea kwa urahisi na hivyo kumpatia hasara mkulima.

"Kama ambavyo mnaona hili shamba darasa mazao yamekuwa vizuri kutokana na matumizi ya mbegu bora na pembejeo nzuri"alisema


Meneja wa Kanda ya kaskazini wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea ,Gothad Liampawe alisema kuwa mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani ni kipindi cha kilimo .

Alisema mamlaka hiyo imejitahidi kudhibiti uingizwaji wa mbolea feki ili kumkwamua mkulima na athari za matumizi ya mbolea zisizo na ubora.

“Udhibiti wa mbolea uko vizuri kwani serikali imetoa ruzuku kwa mbolea ambapo mkulima aliyejisajili kwa ngazi ya Kijiji anapatiwa mbolea ya ruzuku"alisema

Alisema mbolea ya ruzuku inapunguzagharama uzalishaji na kuongeza kipato cha familia na kupata mazao bora

Baadhi ya wakulima na wauzaji wa pembejeo wakizungumza katika maonesho hayo walipongeza a kampuni ya BALTON Tanzania ambao ni waagizaji na wasambazaji wa mbegu nchini.

Saidi Bakari Hamza kutoka Pemba na Masudi Salimu Nasoro kutoka Unguja walisema wamejifunza  kutambua mbegu bora kulingana na maeneo waliyotoka na kuahidi kwenda kutoa ushauri kwa wakulima wa maeneo yao.

‘’Kumekua na changamoto kwa wakulima tunaowahudumia kule pemba pindi unapowauzia mbegu waliyohitaji 

Meneja mkuu wa kampuni ya Balton Tanzania Jacob vorster  alisema waliamua kuwaita wakulima hao na wasambaji wa mbegu katika mafunzo hayo ili kuongeza ujuzi wa mbegu na kilimo.

Alisema wanataka kuona kilimo.ambacho kina tija katika maeneo yao na kufanikisha malengo ya mkulima kupata mazao mengi na bora baada ya kutumia mbegu bora.

Alisema kufanya kilimo chenye tija katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi kutapelekea nchi kuwa na chakula cha kutosha na pia kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja.

Awali akifungua maonesho hayo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu nchini (TASTA) Bobu Shuma aliwataka wakulima na wauzaji mbegu kushirikiana.

Alisema wakulima  waanatakiwa kupata ushauri wa mbegu bora inayofaa kulingana na mahali wanapolima kuendana na mazingira ya hali ya hewa.


"Lazima wauzaji ña mbegu mshirikiane na wakulima ili muwasaidie   kupata mazao bora na kuepuka hasara ya kutumia mbegu zisizo na ubora"alisema

Alisema pia wakulima wanapaswa kufuata ushauri wa wataalam wa kilimo na udongo ili kuongeza uzalishaji.

Wakulima na mawakala.wa pembejeo zaidi ya 400 walishiriki katika maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI