Header Ads Widget

WAJASIRIAMALI WA MSIKITI WA MTOLO KARIAKOO WAUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA KUCHANGIA DAMU


Umoja wa Wajasiriamali zaidi ya 70 wa mtaa wa Zigua na Mahiwa Kariakoo maeneo ya Msikiti wa Mtoro wamejitolea damu kwaajili ya maandalizi ya kuingilia mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni mwezi 28 Shaban1446 AH kwa lengo la kuchangia Banki ya damu salama ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara katika Mitaa ya Mahiwa  na Zigua Simba Issa Lichanda kabla ya kuanza zoezi  la utoaaji wa damu Afisa kutoka Kitengo cha Damu Salama amesema kuwa  anawapongeza  waumini  wa dini ya Kiislamu kwa sababu wamekuwa  mstari wa mbele na wana rekodi ya kuongoza kwa uchangiaji wa damu nchini .

"Nawapongeza  ninyi mnawito na takwimu  zenu za uchangiaji zipo kwenye benki ya damu" amesema.

Pia nachukua fursa hii kutoa pongezi zangu kwa UWAMIK kwa kuhamasishana na kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu  kwani duniani hakujawahi kuwa na mbadala wa amu ieleweke hivyo.

Naye Imamu  Mkuu wa Msikiti wa Kwamtoro Ramadhan Abbas uliopo kati ya mitaa ya Mahiwa na Zigua  amesema kuwa  kutoa damu kwa hiari ni jambo la ibada katika imani huku akitoa wito kwa waumini wake kujitoa kwa ajili ya sadaka hiyo ambayo itawafaa wengine wenye uhitaji kama kima mama wajawazito na wagonjwa wengine walioko mahospitalini wenye kuhitaji  damu.

















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI