Na Shomari Binda-Musoma
JUMUIYA ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi ( UWT) mkoa wa Mara imedhamiria kufanya ziara kila Wilaya kuelezea mafanikio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tangu alipoanza kuongoza nchi.
Ziara hizo zimekusudia kufanikisha kupata kura za kishindo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu kuanzia kwa Rais,wabunge na madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mara Nancy Msafiri amesisitiza umuhimu wa kufanya ziara hizo leo machi 20,2025 kwenye kikao cha baraza la jumuiya hiyo mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara.
Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka 4 amefanya kazi kubwa isiyo tegemewa na wengi hivyo lazima wananchi waelezewe waweze kumuelewa na kumchagua kwa kishindo.
Nancy amesema Rais Dkt.Samia amewaheshimisha wanawake kwa usimamizi wake na uongozi bora ambao shukrani kwake ni kumchagua kwa kishindo.
Amesema Rais Dkt.Samia ametoa fedha nyingi kwa mkoa wa Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyowanufaisha wananchi.
Katika baraza hilo lililohudhuliwa pia na madiwani wa viti maalum wa mkoa wa Mara Mwenyekiti huyo amehimiza kupita kwenye maeneo yao kuelezea mafanikio hayo.
" Twende tukafanye ziara kwenye maeneo yetu kuelezea kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt.Ssmia Suluhu ambayo kila mmoja anaiona.
" Tunataka tumpe shukrani nyingi kupitia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa ndio mgombea wetu na kutufanyia kazi kubwa na ndio maana tumewaalika viongozi wa dini kumuombea Rais wetu",amesema.
Aidha baraza hilo limetoa vyeti vya pongezi kwa Wilaya ambazo zilifanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na kuahidi zawadi kubwa kwa watakaofanya vizuri kwenye uchaguzi wa 2025.
Pia kupitia baraza hilo viongozi wa dini kupitia kamati ya malidhiano wamemuombea dua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa miaka 4 ya uongozi wake na kuendelea kuliongoza Taifa.
Wakati huo huo Katibu UWT mkoa wa Mara Zaidan Mwamba ametoa barua za katazo la uandaaji wa vikao visivyo rasmi kuelekea uchaguzi wa oktoba 2025.
0 Comments