Header Ads Widget

TRA YAKUSANYA TRILLION 21.20 KWA MIEZI NANE

 


NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA DODOMA

KATIKA  kipindi cha miezi nane kuanzia mwezi Julai 2024 mpaka Februari 2025, 

TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh. trilioni. 21.20 sawa na ufanisi wa 

asilimia 104, ya lengo la kukusanya sh. trilioni 20.42; ambao ni ukuaji wa 

asilimia 17 ukilinganisha na kiasi cha sh. trilioni 18.06 kilichokusanywa 

kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita, 2023/24. 


Hayo yameelezwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Machi 12, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.



Amesema Makusanyo hayo ni 

sawa na ongezeko la sh. trilioni 9.28 ambalo ni ukuaji wa asilimia 78

ukilinganisha na kiasi cha sh. trilioni 11.92 kilichokusanywa kipindi cha mwezi Julai 2020 mpaka Februari 2021, kabla ya Mhe Rais kuingia madarakan


Amesema kwa kipindi cha miaka minne ya Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT, akiwa madarakani, makusanyo ya kodi yanayokusanywa na TRA yameongezeka kwa asilimia 78, kutoka Tshs. Trilioni 11.92 hadi Tshs. Trilioni 21.20.


Katika miezi minane (8) ya kwanza kwa mwaka wa Fedha 2024/25, TRA 

imefanikiwa kuvuka malengo iliyopangiwa na serikali kwa kila mwezi 

kwa miezi yote minane mfululizo (clean sheet).


Hata hivyo TRA imeweza kushirikiana na Viongozi wa vyama vya wafanyabiashara nchini kujenga mahusiano na kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kibiashara na kikodi za wafanyabiashara.



"Tumefanya vikao vya pamoja na walipakodi wa ngazi zote yaani wakubwa, wa kati na wadogo (Taxpayers’ Engagement Programs) kwa kuwafuata walipo mikoa yote ya JMT, ambapo changamoto mbalimbali za walipakodi zimekuwa zikitatuliwa haraka ili kupunguza malalamiko, " Amesema


USHIRIKIANO KATI YA TRA NA WALIPAKODI


Hata hivyo amesema wametenga kila Alhamisi ya wiki kama siku maalumu ya kusikiliza na kutatua changamoto za walipakodi. 


"WITO wetu ni kuwaomba walipakodi kutumia siku hii maalumu kukutana na viongozi wa TRA nchi nzima- District Manager, Regional Manager , Makamishna na Wasaidizi wao ili kutatua changamoto zao za kikodi., "


Pia wanaendelea kuimarisha Ushirikiano na viongozi wa Serikali, viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa michezo (TFF) na wasanii mbalimbali.


Kuwezesha kukua kwa Biashara na Shughuli za Kiuchumi nchini

Kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo kurahisisha taratibu za ulipaji kodi na kupunguza urasimu. 


"Hatua hizi zimevutia wawekezaji na kuongeza wigo wa walipakodi na hivyo kuongeza mapato ya serikali,

Tumerahisisha sana utoaji wa vivutio vya Kodi kwa wawekezaji katika ofisi zetu zote, " Amesema. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI