Header Ads Widget

KIBONDO YAPIGA HATUA UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI


Na Fadhili Abdallah

Halmashauri ya wilaya Kibondo mkoani Kigoma inaelezwa kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ambazo zimeiwezesha halmashauri hiyo kuweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni tatu katika mapato yake ya ndani.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kibondo, Diocles Rutemwa alisema hayo akitoa taarifa ya hali ya utendaji ya halmashauri hiyo kwa Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM,Abdulkadri Mushi aliyekuwa akiongoza kamati ya siasa ya mkoa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.

Rutema alisema kuwa halmashauri imetekeleza miradi ambayo imesaidia kuongeza mapato ya ndani ambapo kwa sasa halmashauri inaweza kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni tatu kutoka kukusanya kiasi cha shilingi mlioni 400 mwaka 2020 na hivyo kuweza kutekeleza miradi mikubwa kwa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.

Akieleza mafanikio hayo ya halmashauri Mkuu wa wilaya Kibondo,Kanali Agrey Magwaza alisema kuwa yanatokana na serikali wilayani humo kupokea  kiasi cha shilingi bilioni 46.4 zilizotolewa na serikali kutoka kiasi cha Shilingi trilioni 11.5 ambazo zimepokelewa mkoani humo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati.

Akihitimisha ziara yake wilayani Kibondo Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa Kigoma,Abdulkadri Mushi akiongoza wajumbe wa kamati siasa ya mkoa Kigoma alisema kuwa fedha zinazoletwa na serikali kwenye halmashauri ni lazima zionyeshe kwa vitendo matokeo chanya katika maendeleo ya vitu na watu hasa manufaa yake katika maisha ya wananchi wa kawaida.



Diocles Rutema Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya Kibondo 


Abdulkadri Mushi Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM


Kanali Agrey Magwaza Mkuu wa wilaya Kibond


Mjumbe wa halmashauri kuu ya Tifa ya CCM Abdulkadri Mushi akiwaongoza wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa Kigoma kutembelea na kukagua miradi wilayani Kibondo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI