Header Ads Widget

GULAMALI ATUNUKIWA CHETI CHA HESHIMA NA IGP


Na Baraka Mashauri, Matukio Daima App-Tabora. 

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Camillius Wambura amemtunukia cheti cha heshima Mbunge wa Jimbo la Manonga Wilayani Igunga Mkoani Tabora Sief Hamis Gulamali kwa mchango wake mkubwa wa kuchangia ujenzi wa kituo cha Polisi Kata ya Nkinga Tarafa Simbo.

Amekabidhiwa cheti hicho wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha Polisi kilicho jengwa kwa nguvu ya mbunge huyo kwa kushilikiana na Wananchi wa kata hiyo ujenzi ulioghalimu kiasi cha shilingi 81,075,000 ambapo kita hudumia jumla ya wakazi wa kata zipatazo tano, ambazo ni kata ya Nkinga, Kitangili, Ndembezi, Ugaka na Mwisi, ambozo kwa pamoja zina jumla ya wakazi 56,739.

Akikabidhi cheti hicho na kufungua kituo hicho kipya cha Polisi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha, Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo amesema kuwa wananchi wana wajibu wa kujiletea maendeleo mbali na maendeleo yanayoletwa na Serikali, hivyo kukakimila kwa kituo hiki ni maendeleo yaliyoletwa na wananchi wenyewe jambo ambalo linakwenda kuwainua kiuchumi kwani sasa jimbo la Manonga linakwenda kuwa na amani. 

" kwa kushirikiana na viongozi wetu ndio maana tukawiwa na kuona umuhimu wa kuimarisha suala zima la ulinzi na usalama katika kata yetu kwa kujenga kituo hiki, kituo bora na cha kisasa tunawapongeza sana, na sisi kama Serikali tunawapongeza wale wote walioguswa na kuchangia katika ujenzi wa kituo hiki, " alisema DC Mtondoo. 

Akipokea Cheti hicho Mbunge wa Jimbo la Manonga Mhe. Seif Gulamali amewapongeza wananchi na mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Nkinga kwa ushirikiano wao ambao umewezesha kutunukiwa cheti cha heshima na IGP. 

" Kupitia michezo tumetoa elimu mbalimbali na kuwaunganisha wananchi na jeshi la Polisi na kupunguza uhalifu, Mkuu huyu wa kituo anapo hamishwa kwenda kituo kingune wananchi wamekuwa wakimlilia," alisema Gulamali.

Aliendelea kusema kuwa, " Wilaya nzima ya Igunga yenye kata 35 hata makao makuu yetu ya wilaya anapotoka ndugu yetu OCD hawana kituo kama hiki, nipende kuchukua nafasi hii mgeni rasmi kukuambia kuwa wananchi wa Jimbo la Manonga wamekuwa wanajitolea kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali sio tu huu wa kituo hiki cha Polisi."

Aidha, Mbunge Gulamali amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kwa kuwangu mkono wananchi wa Jimbo la Manonga kwa miradi mbalimbali, Sanjali na hayo mbunge Gulamali ametoa pikipiki tatu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi ambapo pikipiki mbili zitatumiwa katika kituo kipya cha Polisi Nkinga na Pikipiki moja itatumika katika kituo kidogo cha Polisi kata ya Simbo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao ametoa maelelekezo kwa Askari wote mkoa wa tabora kushirikiana kwa ukaribu na wananchi na kuakikisha wanafanya kazi kwa Mujibu wa sheria na taratibu za jeshi la polisi

"Nimekuwa nikija mara kwa mara kuangalia ujenzi huu haujawahi kuwa na nyufa wala matobo ujenzi wake umakuwa na ubora tukea mwanzo mpaka mwisho hatujawahi kuziba nyufa kwa hiyo hiki ni kituo bora kabisa kama mgeni rasmi ulivyo kikagua,"

Kamanda Abwao alisema kuwa, " Tulimtumia picha Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Wambura na amewapongeza na kuwashukuru sana, kwa sasa tunatoa huduma bora kwa wananchi kwani pale wanapoleta malalamiko kwa Jeshi la Polisi tunahakikisha tunamsikiliza na anaondoka ameridhika,"

Kwa upande wao wananchi wakizungumza baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho cha Polisi wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Manonga Mhe. Seif Gulamali kwa kuwaunganisha wananchi na Jeshi la Polisi sambamba na kutoa pikipiki tatu zitakazo saidia kuatuka kupambana na kuzuia uhalifu katika Jimbo hilo.

Akizungumza kwa naiaba ya wananchi wenzake Haji Yange amemshukuru Mhe mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali kwa kujengea kituo cha Polisi. 

"Katika kata yetu ya Nkinga kwani amekuwa anajitoa kuunganisha wananchi, kituo hiki ni cha mfano kwa Taifa zima kwani wananchi wamejitoa ila kwa asilimia 80 mbunge amejitoa," alisema Haji Yange.

Naye Mwigulu Kulwa aliitoa pongezi kwa Mh. Gulamali, kwa Mkuu wa wilaya Sauda Mtondoo na kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kwa jitihada zao za kujenga kutuo bora Jimboni Manonga kwani kitatoa ufanisi na kwenda kudhibiti uhalifu.

" Tunamshukuru pia Mbunge kwa kutoa Pikipiki Tatu kwa maana hiyo ulinzi katika jimbo letu la Manonga unakwenda kuimalishwa kwa sababu tumepata vitendea kazi vya kupata taarifa za uhalifu na wahalifu jambo ambalo watakwenda kushughulikiwa kwa haraka," alisema Kulwa.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI