Header Ads Widget

DAWASA YATEKELEZA MIRADI YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

 

 

Na Hamida Ramadhan Dodoma

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikiwa kutekeleza miradi zaidi ya ishirini na tano yenye thamani ya Tsh bilioni 987.6 Kuanzia Julai 2021, 

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 11, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Amesema Kati ya miradi hiyo, Tsh bilioni 232.9 zimekamilika na sasa zinatoa huduma kwa jamii, wakati Tsh bilioni 754.7 bado ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Ameeleza kuwa, DAWASA pia imeandaa miradi mipya yenye thamani ya Tsh trilioni 3.1, ambayo inajumuisha gharama za usanifu, ujenzi, upanuzi, na ukarabati wa miundombinu ya maji na majitaka. Fedha hizi zinatokana na makusanyo ya DAWASA, Serikali kuu, na mikopo ya masharti nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, ikiwa ni pamoja na Benki ya Dunia na Serikali za Korea Kusini na India.

"Katika hatua za maendeleo, uwezo wa uzalishaji maji umeongezeka kutoka lita 520,000,000 hadi 534,600,000 kwa siku, na uwezo wa kuhifadhi maji umeongezeka kutoka lita 153,649,000 hadi 198,965,000," Amesema Mhandisi Bwire

Aidha amesema , mtandao wa usafirishaji na usambazaji maji umeongezeka kutoka kilomita 4,690.7 hadi 7,206, na mtandao wa majitaka umeongezeka kutoka kilomita 450 hadi 519.4.

 

Kwa upande wa huduma amesema , idadi ya maunganisho ya wateja wa majisafi imeongezeka kutoka 343,019 hadi 455,720, na upatikanaji wa huduma za maji umeongezeka kutoka asilimia 89 hadi 93. 

"Huduma za usafi wa mazingira zimeimarishwa, zikiongezeka kutoka asilimia 25 hadi 45," Amesema Mhandisi Bwire.

Pia ameelezea Mradi mkubwa wa bwawa la Kidunda, wenye thamani ya Tsh bilioni 335.9, umefikia asilimia 28 katika utekelezaji, huku Tsh bilioni 85.4 zikiwa zimetolewa hadi sasa. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI