Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe chini ya Mwenyekiti wake Deo Sanga Kimelaani vikali tukio la kupigwa kwa katibu Mwenezi wa Baraza la wanawake Chadema Taifa Sigrada Mligo kilichofanywa Machi 25 Mwaka huu na anayedaiwa kuwa ni mlinzi wa Chama hicho wakati wa vikao vya ndani.
Uongozi wa CCM mkoani Njombe umelaani kitendo hicho ulipofika Katika Kijiji Cha Kisilo kata ya Lugenge Halmashauri ya mji wa Njombe Nyumbani kwa Sigrada baada ya maelekezo ya Katibu mkuu wa CCM Taifa kupitia kwa Mwenezi wao Amos Makala na kwamba jambo Hilo linapaswa kupigwa vita na kila mtanzania.
Awali katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter amesema baada ya maelekezo ya CCM taifa wamefika Nyumbani kwa Sigrada na kumjulia hali huku wakiwataka watanzania kuendelea kudumisha amani badala ya kuendekeza ugomvi na vurugu.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Baraza la wanawake Chadema Taifa Sigrada Mligo anasema kwa sasa anaendelea vizuri huku akishukuru uongozi wa CCM kwa kufika nyumbani na kumjulia hali.
Jumuiya ya wanawake wa CCM mkoa wa Njombe UWT chini ya Mwenyekiti wake Dokta Scholastica Kevela akiwa Kijijini hapo naye amelaani vikali tukio la kupigwa kwa mwanamke mwenzao na kulitaka jeshi la Polisi kuchukua hatua za kumsaka na kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.
Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Njombe chini ya Kamanda wake Mahamoud Banga limesema linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo aliyekuwa miongoni mwa walinzi katika Kikao Cha makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa John Heche alipozulu mkoani Njombe kwa ajili ya mikutano yao ya hadhara.
MWISHO.
0 Comments