Header Ads Widget

BUWSSA YAZUIA UPOTEVU WA MAJI KWA ASIMIA 32 KUTOKA ASIMIA 64


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

MKURUNGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji wa Bunda (BUWSSA) Esther Gilyoma amesema Upotevu wa maji kwa sasa ni asilimia 32 toka wastani wa asilimia 64 mwaka 2021 kutokana na mtambo wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972, 


Ameyasema  hayo Leo jijini Dodoma wakatia akiongea na wandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka minne ya matanikio ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan 

Amesema baada ya jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya sita (6) za kutoa fedha za kubadili bomba chakavu na mita goigoi upotevu wa maji kwa  na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika. 

UPATIKANAJI WA MAJI NA MASAA YA HUDUMA

Amesema Kwa mwaka 2021 Mamlaka ilikuwa inatoa huduma yam aji kwa wastani wa masaa 12 kutokana na ufinyu wa mtandao na kutokuwa na maji ya kutosha,kwa mwaka 2023 baada ya mradi mkubwawa kusafisha na kutibu maji Nyabehu Bunda kukamilika.

"Kwa sasa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda inatoa huduma ya majisafi kwa wastani wa masaa 22 bila ya kuwa na mgawo wa maji, baada ya miradi miwili kukamilika ambayo kwa sasa inaendelea mradi wa kusambaza maji Wariku na mradi wa maji Kisangwa, " Amesema

Na kuongeza "Mamlaka itatoa huduma ya maji kwa masaa 24 na kufikisha wastani wa utoaji wa huduma kwa wastani wa asilimia 96 na kufikia lengo la ILANI ya chama cha mapinduzi (CCM)," Amesema.

Aidha Katika hatua nyingine Mamlaka ya maji Bunda kupitia kitengo cha huduma kwa wateja kina huduma kwa wateja (call cetre) ambapo malalamiko ya wateja uchukuliwa na kufanyiwa kazi ndani ya masaa 24,pia elimu kwa wateja na ushirikishwaji kwa wadau hutolewa kupita vyombo vya habari,matangazo na mikutano mbali mbali nia ikiwa ni kujenga uelewa wa pamoja na wadau wa maji na kuboresha huduma ya maji.

USAFI WA MAZINGIRA 

Mkurugenzi huyo amesema Kutokana na jitihada za kupambana na usafi wa mazingira Bunda, kwa sasa Mamlaka ya maji Bunda ina ujenzi wa mradi wa miundo ya majitaka katika eneo la Butakale kwa ajili ya usafi wa mazingira, mradi huu unatarajia kukamilika kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025.Mradi huu una ununuzi wa magari mawili ya majitaka yenye uwezo wa kubeba lita 10,000 na 5,000.

Hata hivyo Mamlaka ina jumla ya wateja 9,318 kwa sasa ambapo kwa mwaka 2021 Mamlaka ilikuwa na jumla ya wateja 5,149 ambao ni watumiaji wa majumbani (Domestic), Biashara(Commercial), Taasisi (Institution), na Viula(viosk). 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI