Header Ads Widget

WANANCHI WAMEHIMIZWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA SARATANI WALAU MARA MOJA KWA MWAKA

 


Wananchi wamehimizwa kujenga utamaduni wa kupima Saratani walau mara moja kwa mwaka ili kujua hali zao za kiafya ili kuepukana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza hapo baadae.


Hayo yamesemwa leo tarehe 4 Februari, 2025 na Mhe. Beno Malisa Mkuu wa wilaya ya Mbeya “mgeni rasmi”  akiongea kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera kwa wananchi waliojitokeza kupima afya zao katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani iliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.


“…nitumie fulsa hii kuwaomba wananchi wa mkoa wa Mbeya tuwe na utamaduni wa kupima afya zetu walau mara moja kwa mwaka ili kuona dalili za awali zinazosababisha  usiingie katika changamoto kubwa” – Mhe. Beno Malisa


Aidha Mhe. Beno Malisa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa maboresho mbalimbali ya miundombinu ya huduma za matibabu ya Saratani yaliyofanywa ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya sambamba na kuwapongeza watumishi wa Hospitali kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuwahudumia wagonjwa wa Saratani.


“…tunamshukuru sana Mhe. Rais kwa kendelea kuboresha miundombinu ya afya kwa kuhakikisha watu wetu wote wanakuwa na afya ya mwili pamoja na akili” – Mhe. Beno Malisa


Akisoma Lisara kwa niaba ya watumishi wa Kitengo cha Saratani Hospitalini hapa Dkt. Tibela Lugambwa amesema, kati ya watu kumi wanaogundulika na Saratani, watu wanne hupoteza maisha ambapo kwa upande wa saratani zinazoongoza kwa watu wazima ni pamoja na Saratani ya Shingo ya Kizazi, ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa wanawake, saratani ya tezi dume na saratani ya mfumo wa chakula, na kwa upande wa watoto ni saratani ya damu, saratani ya figo, saratani ya macho, saratani ya tezi na saratani ya mifupa.


“…kwa takwimu za mwaka 2022 inayonyesha kwamba takribani watu 45,000 wanagundulika na saratani nchini, kati hao, watu 17,000 hupoteza Maisha kwa maneno mengine kati ya watu kumi wanaogundulika na saratani watu wanne hupoteza maisha”- Dkt. Tibela Lugambwa


Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwepo wa idara ya Saratani hospitalini hapa kwani kwa muda mrefu wananchi walitakiwa kusafiri umbali mrefu kwenda kupata matibabu ukilinganisha na sasa ambapo wananchi wamepunguziwa gharama kubwa kutokana upatikanaji wa huduma hii mkoani Mbeya.


“…kipekee sana tuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani idara ya saratani hospitalini hapa ni idara mpya, kwa muda mrefu wananchi wa Nyanda za Juu Kusini iliwalazimu kwenda Dar Es Salaam kupata matibabu ya ugonjwa huu” – Dkt. Mbwanji


Kwa upande wake Miriam Olomi mnufaika wa huduma ya matibabu ya Saratani ya Titi Hospitani hapa “shujaa wa Saratani” amewaasa wananchi kujenga tabia ya kupima saratani mapema kwani endapo itagundulika mapema inatibaka.


“… saratani inatabika endapo itatibiwa mapema kwani kuna watu wanawaficha wagonjwa wa saratani kwa kuogopa jamii itawachukuliaje” – Miriam Olomi.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI