TAZAMA HABARI NZIMA YA WASHTAKIWA MAUAJI YA KATIBU CCM KILOLO BOFYA LINK HII
NA BERDINA MAJINGE, MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA
MAHAKAMA ya wilaya ya Iringa imeahirisha Kesi ya ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Christina Kibiki hadi mpaka February 17,2025 itakapo tajwa tena baada ya kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Akiomba kuahirishwa kwa kesi hiyo leo wakili wa serikali Atupele Makoga alisema kuwa wanaomba kesi hiyo ipangwe siku nyingine ili waweze kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Kwa upande wake wakili wa utetezi Barnabas Nyalusi kutoka kampuni ya mawakili ya BLS Attorney &Partner ameimba Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Iringa kuwahimiza upande wa Jamhuri kuharakisha upelelezi wa Kesi hiyo kwani karibu siku 90 walizopewa kisheria zinaisha.
Wakili Nyalusi alisema mbele ya mahakama kuwa kesi hiyo inasikilizwa na kufatiliwa na jamii kwa ukaribu hivyo ni vyema mchakato wa upelezi ukakamilika haraka ili ianze kusikilizwa.
Kutokana na maombi hayo ya upande wa Jamhuri hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Iringa Adelina Faustino Ngwaya aliahirisha Kesi hiyo
Waliofikishwa Mahakamani hapo ni pamoja Boniphace Yohana Ugwale ambae ni diwani wa kata ya Nyanzwa Kilolo Kefa John Wales,Silla Johnson Kimwaga,Boniphace Yohana Ugwale katili ,Willy Gerald Chikweo na Hedikosi Gwerino Kimwaga kwa pamoja wanashitakiwa kumuua Christina Kibiki.
Washitakiwa hao walitenda kosa hilo mauaji Novemba 12 mwaka 2024 katika Kijiji Cha Ugwachanya wilaya ya Iringa Vijijini.
MWISHO.
0 Comments