Header Ads Widget

VALENTINE DAY YANOGESHWA NA DIKO LA AMBONI TANGA


Na Philomena Mbirika, Amboni Tanga.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imehitimisha Kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mapango ya Amboni, Tanga Leo tarehe 14 Februari, 2025 ambapo  wananchi mbalimbali walihamasika kufanya utalii wa ndani katika siku ya wapendanao (Valentine day)  na kufurahia pishi la vyakula vya asili hasa kwa watu wa Tanga.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha Kampeni ya kuhamaisha utalii wa ndani katika eneo la Mapango iliyoambana na mashindano ya Mapishi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh. Japhari Kubecha ameupongeza uongozi wa NCAA kwa Ubunifu ambapo kupitia kampeni imeongeza  hamasa kubwa ya utalii wa ndani katika mkoa wa Tanga.

“Niendelee kuipongeza NCAA kwa ubuhifu wao mkubwa wa kukuza utalii ndani ya Mapango ya Amboni. Niwaahidi kwamba serikali ya Wilaya ya Tanga itaendelea kushirikiana na nyie kuendeleza na kutunza mapango haya ya pekee” Alisema Mhe. Kubecha

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia huduma za utalii na Masoko NCAA, Mariam Kobelo alisema kwamba  NCAA inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya Mapango hayo ili yaendelee kuvutia watalii wengi zaidi.

“Kwa sasa tuna mpango wa utekelezaji wa mikakati  mbalimbali ikiwemo kuboresha  miundombinu, mfumo  ukusanyaji wa mapato, kujenga maeneo ya kupumzika pamoja na uwekwaji wa kambi kwa wageni watakaopenda kulala hapa”. Alisema Mariam 

Kobelo alieleza kuwa kuhitimisha Kampeni hiyo kwa mashindano ya mapishi itasaidia kutoa fursa ya kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo ndani ya Wilaya ya Tanga.

Washiriki wa mashindano hayo ya upishi walipewa zawadi na NCAA ambapo ikijumuisha fedha taslimu pamoja na mitungi ya gesi kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.








#visitamboni #dikolaamboni

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI