Header Ads Widget

TANZANIA ,CUBA KUSHIRIKIANA UHIFADHI ENDELEVU

 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Cuba zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya utalii na uhifadhi wa wanyamapori hasa kukabiliana na changamoto ya mimea vamizi ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa.


Hayo yamejiri Februari 16,2025 katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ujumbe wa Cuba uliongozwa na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Cuba, Mhe. Humphrey Polepole na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera na kwa Tanzania ujumbe ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb).

 

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewakaribisha wataalamu saba kutoka nchini Cuba waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tafiti ya kina kuhusu changamoto ya mimea vamizi inayozikabili hifadhi mbalimbali za taifa na maeneo mengine yaliyohifadhiwa lengo ikiwa ni kutafuta ufumbuzi wa uhakika katika kukabiliana na changamoto hizo.


“Napenda kutambua kwamba, mimea vamizi ni tishio kubwa la uhifadhi nchini Tanzania, hasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro na Bonde la Ziwa Victoria. Spishi hizi, asilia na ngeni, zimevuruga mifumo ikolojia, mimea asilia iliyohamishwa, na kuathiri vibaya makazi ya wanyamapori, utalii, ardhi ya malisho na jamii za wenyeji. Spishi hizi vamizi zimeharibu mazingira na kuathiri utalii” amesisitiza Mhe. Chana.


Amefafanua kuwa uwepo wa mimea vamizi ulisababishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli za kibinadamu, kama vile kilimo, biashara ya mimea ya mapambo, na mipango ya kudhibiti mmomonyoko wa udongo.


Kupitia wataalam hao kutoka Cuba, Tanzania itapata utaalamu wa teknolojia bora ya kukabiliana na mimea vamizi na kuendeleza uhifadhi nchini .







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI