Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka viongozi na wataalamu Mkoani humo kutafsiri vema na kwa vitendo maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya ili iwe na tija kwa jamii hususani katika kuinua ufaulu wa wanafunzi kwenye shule ambazo hazifanyi vizuri
Chalamila amesema hayo leo Feb 11,2025 wakati akizungumza Wilayani Temeke Jijini katika mkutano na wadau mbalimbali wa elimu amesema Serikali chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikiimarisha miundombinu ya elimu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia hivyo ni muhimu kwa kila mdau wa elimu ikiwemo wazazi, viongozi pamoja wataalamu kujielekeza kwenye kusaidia watoto ili kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi
Aidha Chalamila amesema kuwa badala ya kutazama sababu chache zinazotolewa na kuonekana kusababisha ufaulu kuwa hafifu ni muhimu kufanya utafiti wa kina na kuhakikisha wazazi wanashirikishwa ipasavyo kwenye kuinua ufaulu wa wanafunzi ili ndoto za Rais Dkt Samia zitimie na fedha nyingi anazozitoa kuimarisha miundombinu ya elimu zitimize lengo husika.
Vilevile Chalamila amesema hivi karibuni Serikali Mkoani humo inatarajia kufanya mkutano utakaojumuisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili kujadili kwa pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa wazazi kwenye masuala ya elimu.
0 Comments