Header Ads Widget

MIAKA 48 YA MIAKA 48 YA CCM NI USHINDI WA DKT. SAMIA UCHAGUZI MKUU – FESTO KIPATE NI USHINDI WA DKT. SAMIA UCHAGUZI MKUU – FESTO KIPATE

 

Na Matukio Daima media 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeadhimisha miaka 48 kikiwa thabiti, kikiwa na historia ya mafanikio makubwa katika maendeleo ya nchi. Katika kipindi hiki, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kuwa chachu ya maendeleo, uthabiti wa kisiasa, na mshikamano wa kitaifa.

Mdau wa maendeleo kata ya Ukumbi  wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kada wa CCM Festo John Kipate akizungumza na Matukio Daima Tv jana katika kipindi Cha jukwaa la Siasa alisema kuwa Dkt. Samia ameweza kujenga chama na kuimarisha utawala bora kupitia falsafa yake ya 4Rs (Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding). 

Pia meweza kutekeleza  miradi mikubwa ya maendeleo, utendaji wake katika nyanja mbalimbali, na jinsi ambavyo Watanzania wanapaswa kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao.

Kipate alisema toka  alipoingia madarakani mwaka 2021, Dkt. Samia ameonesha uwezo mkubwa wa uongozi kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea katika mstari wa maendeleo. 

"Kupitia falsafa yake ya 4Rs, ameweza kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja za siasa, uchumi, na jamii Reconciliation (Maridhiano)"

Kuwa Dkt. Samia amefanikisha maridhiano ya kisiasa kwa kufungua milango ya mazungumzo kati ya vyama vya siasa. Hatua hii imesaidia kupunguza migogoro ya kisiasa na kujenga mazingira ya demokrasia shirikishi.

Pia ameziba pengo la tofauti za kisiasa kwa kuruhusu vyama vya upinzani kushiriki kwenye majukwaa ya kisiasa kwa uhuru zaidi, tofauti na miaka ya nyuma.

Kuhusu Resilience (Ustahimilivu)Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imepitia changamoto mbalimbali, ikiwemo athari za janga la UVIKO-19 na mfumuko wa bei duniani.

Kuwa Dkt. Samia ameonesha ustahimilivu kwa kuweka mikakati ya kufufua uchumi, ikiwemo kuongeza uwekezaji, kuboresha mazingira ya biashara, na kuimarisha sekta ya afya ili kukabiliana na majanga ya kiafya.Reforms (Marekebisho)Serikali yake imefanya marekebisho makubwa katika sekta za sheria, uchumi, na utawala bora.

"Ametekeleza mageuzi makubwa katika utawala wa fedha za umma, kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali na kupambana na ufisadi.Rebuilding (Ujenzi Upya)Dkt. Samia ameendeleza ujenzi wa miundombinu mikubwa kama barabara, reli, na viwanja vya ndege, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuiimarisha Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa Afrika Mashariki."alisema Kipate 


Kuwa Katika kipindi chake cha uongozi, Dkt. Samia amehakikisha kuwa miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi. Baadhi ya miradi kama ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaendelea kwa kasi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha usafirishaji wa abiria na mizigo,mradi wa barabara kuu na madaraja makubwa umeendelea kuimarisha usafiri na uchukuzi ndani ya nchi na kuunganisha mikoa mbalimbali.

"Serikali yake imeongeza bajeti ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari Ujenzi wa shule mpya na vyuo vya ufundi umeongeza fursa za elimu kwa vijana wengi nchini"


Kipate anasema upande wa sekta ya Afya Hospitali mpya zimejengwa katika mikoa na wilaya mbalimbali, kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi.

Pia Serikali imeongeza bajeti ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote.


Hata hivyo hakuishia hapo upande wa Sekta ya Nishati Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere (JNHPP) unaendelea kutekelezwa ili kuongeza uzalishaji wa umeme wa kutosha kwa matumizi ya viwanda na wananchi,Mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia REA umewezesha vijiji vingi kupata nishati ya umeme, kusaidia ukuaji wa uchumi vijijini.

Mdau huyo wa maendeleo wilayani mkoani anasema Kwa upande wa Sekta ya Kilimo na Mifugo Serikali imewekeza katika ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji ili kusaidia wakulima kuzalisha mazao kwa wingi na kwa ufanisi zaidi.Wafugaji wamepata msaada wa pembejeo bora na huduma za afya ya mifugo, kuhakikisha uzalishaji unakuwa wa kisasa na wenye tija".

Alisema Kwa upande wa Siasa kuwa katika historia ya siasa za Tanzania, haijawahi kushuhudiwa maridhiano ya kisiasa kama ilivyo sasa. 

Kuwa Chini ya uongozi wa Dkt. Samia, viongozi wa vyama vya upinzani wametambua mchango wake katika kuleta maendeleo na utawala bora.

"Viongozi wa upinzani wameanza kuunga mkono baadhi ya sera zake, wakikiri kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa chini ya uongozi wake  hili ni jambo la kihistoria, linalothibitisha kuwa Dkt. Samia anapaswa kupewa fursa nyingine ya kuendelea kuiongoza nchi"

Kwa Nini Dkt. Samia Anatosha kwa Uchaguzi Mkuu Ujao?

Alisema kuna sababu nyingi zinazoonesha kuwa Dkt. Samia anastahili kupewa nafasi ya kuendelea kuiongoza Tanzania kama uzoefu na Uwezo wa Uongozi kwani ameshathibitisha kuwa ana uwezo wa kusimamia maendeleo na kuimarisha utawala bora,Mageuzi Makubwa Katika Sekta Mbalimbali kwani ameleta mabadiliko chanya katika uchumi, siasa, afya, elimu, na miundombinu pamoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Kwani Dkt Samia tumeshuhudia amejenga taifa lenye mshikamano kwa kupunguza migogoro ya kisiasa na kuboresha mahusiano kati ya serikali na wananchi ,miradi mingi inaendelea kutekelezwa, na ni muhimu aendelee ili kuhakikisha inakamilika kwa ufanisi.

Kipate alisema kuwa kwa kuangalia rekodi ya utendaji wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakuna shaka kuwa amefanikisha maendeleo makubwa ndani ya miaka yake ya uongozi.

Pia kwa  kutumia falsafa yake ya 4Rs, ameleta mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kuelekea maendeleo endelevu.


Kipate ambae ni mkazi wa Mawambala kata ya Ukumbi wilaya ya Kilolo alisema kwa kuwa hata wapinzani wametambua mchango wake, ni dhahiri kuwa uchaguzi mkuu ujao ni fursa ya Watanzania kuthibitisha imani yao kwake kwa kumpa kura nyingi.

Alisema kuwa  Dkt. Samia anatosha kuendelea kuiongoza Tanzania kwa miaka mingine ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea na nchi inazidi kusonga mbele.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI