NA WILLIUM PAUL.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameshiriki mkutano wa nchi 25 zinazolima Kahawa Afrika (G-25) unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JICC) Dar es Salaam.
Lengo la mkutano huo ni kukuza thamani ya Kahawa na kujadili changamoto zinazokabili zao hilo, na kutumia fursa za kupata ajira hasa kwa vijana wa mataifa haya ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya zao la Kahawa.
0 Comments