Header Ads Widget

WENJE AFUNGUKA UHAINI NDANI YA CHADEMA, AWATAJA LISSU, LEMA KUTAKA KUMPINDUA MBOWE



Na.Matukio Daima App, Dar.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Victoria, Mhe. Ezekia Wenje ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Bara amezungumza na Vyombo vya Habari mapema leo Alhamisi Januari 16, 2025 mkoani Dar es Salaam na kufunguka mambo mbalimbali ikiwemo tuhuma za Tundu Lissu na Godbless Lema kuwa na mpango wa kumpindua katika nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Mhe. Freeman Mbowe.

Mhe. Ezekia Wenje amedai kuwa sababu iliyomfanya kupishana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na Godbless Lema ni kukataa kuhusika na mapinduzi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa gerezani akikabiliwa na kesi kubambizwa ya Ugaidi ambayo waliona hatoweza kutoka.

Mhe Ezekia Wenje amesema kuwa, amefunguka kutokana na kauli za Godbless Lema alizozitoa dhidi yake pamoja na Tundu Lissu hivi karibuni katika vyombo vya Habari.

“Godbless Lema alikuwa kiongozi wa kundi lililotaka kufanya mapinduzi ya kumuondoa Mwenyekiti wa sasa wa chama Mhe. Freeman Mbowe katika nafasi ili Lissu awe Mwenyekiti.

"Ni kweli mimi nilikuwa timu Lissu sasa nimejiondoa kwanini, Mwenyekiti Freeman Mbowe alipokuwa gerezani kwa kesi ya ugaidi, Lema na Lissu walianzisha kampeni ya 'Join the Chain', wakachangisha pesa kwa ajili ya baraza kuu na mkutano mkuu" amesema Wenje

Akaongeza kuwa "Walijua Mwenyekiti Mbowe hawezi kutoka gerezani kwa sababu ana kesi ya ugaidi, hivyo ile kampeni yao ililenga Lissu awe Mwenyekiti wa Chadema, nilivyogundua hivyo nikajiondoa, nilikataa usaliti" amebainisha Wenje.

Aidha, ameonesha mashaka ya akili za Lema kumpendekeza Dkt. Slaa endapo Lissu atachaguliwa.

"Mtu kama Dkt. Slaa ameandika kitabu on record ya kuchafua chama chetu kila kona ndiyo leo Lema anajaribu kufikiria ateuliwe kuwa Katibu Mkuu sasa sijui hiki kitabu akiteuliwa anaenda kukichoma moto au ataenda kuandika kingine cha kureverse haya aliyosema kuhusu chama chetu hiyo pia ni swali lingine, sasa hiki kitabu cha nyuma ya pazia leo Dkt. Slaa anaamini kabisa kwamba Tundu Lissu na anampigia Tundu Lissu debe kwamba anafaa kuongoza CHADEMA kwa sasa na sio Freeman Mbowe ukisoma hiki kitabu kuna kurasa tano ambazo zinamzungumzia tu Tundu Lissu Dkt. Slaa ameandika kumuhusu Lissu". Amesema Wenje.

Wenje amebainisha kuwa, yeye anasimama na CHADEMA na sio mtu hivyo ataendelea kuwa Kiongozi na Mwanacha hai wa CHADEMA bila kushawishiwa na mtu.


"Kuna wengi wameondoka CHADEMA, lakini niwapongeze wanaCHADEMA waliovumilia mateso yote mpaka tumefika hapa, ndiyo maana nasisitiza chama hiki ni kikubwa kuliko mtu yeyote, na mimi nilipojiunga CHADEMA, nilijiunga CHADEMA kwasababu ya itikadi za chama na wala sio itikadi za mtu, kiukweli sikumfuata mtu, nimefuata kanuni na misingi ya CHADEMA. Ninasema sitaondoka CHADEMA kwasababu kuna mtu ameondoka, kwasababu sikumfuata mtu nilifuata itikadi ya chama chetu"- Wenje.

Mhe. Wenje amesisitiza katika kampeni zake amezingatia misingi ya haki na bila kumvunjia mtu heshima kama wafanyavyo wengine.


"Sisi katika kampeni yetu hata Mwanza nilisema sitaruhusu mtu yeyote anayeniunga mkono kwenda kumtukana mtu mwingine, kwasababu mwisho wa siku huu uchaguzi utaisha tarehe 21 Januari 2025, kuna siku zingine mbele na maisha yatasonga, leo ukimtukana mtu sana halafu mwaka huu tuko kwenye uchaguzi wa Rais wa nchi, anataka kugombea Urais lakini mmeshamtukana sana, nyie mtakwendaje kumsafisha mtu huyo? Leo ukimtukana mtu sana na kesho akawa Makamu Mwenyekiti au Mwenyekiti wa chama taifa unaendaje kufanya naye kazi?"- amesema Wenje.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI