Header Ads Widget

WAZIRI KOMBO AONGOZA MENEJIMENTI YA WIZARA KATIKA KIKAO NA KAMATI YA BUNGE YA NUU

Na Matukio Daima media 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameongoza Menejimenti ya Wizara katika kikao na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) uliofanyika jijini Dodoma hivi karibuni.

Wakati wa kikao hicho, Mhe. Waziri Kombo, aliwasilisha taarifa  mbalimbali  kuhusu utendaji kazi wa Wizara ikiwa ni pamoja na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara; taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge;  taarifa kuhusu hali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Jumuiya za Kikanda kama SADC;  na taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Kipindi cha nusu mwaka wa Julai hadi Desemba 2024.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Vita Kawawa ilipokea taarifa hizo na kutoa ushauri na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha na kukamilisha utekelezaji wa masuala mbalimbali kwa wakati.

Katika kikao hicho, mbali na Menejimenti ya Wizara, Mhe. Balozi Kombo alifuatana na Naibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) na Mhe. Dennis Londo (Mb.).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI