Header Ads Widget

REKODI YA BINTI MDOGO ZAIDI KUCHEZA TAEKWONDO MLIMA KILIMANJARO YATAMBULIWA NA JARIDA LA "INDIAN BOOK OF RECORDS (IBR)

 


Na. Philipo Hassan

Source: IBR Journal


Jarida la Indian Book of Records la nchini India limemtambua rasmi msichana mwenye umri wa miaka 13 kutoka Alappuzha, Kerala, Anna Mary Njarackaveli, kwa kuweka rekodi ya kipekee ya kuwa msichana mdogo zaidi kucheza Taekwondo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Mlima mrefu zaidi barani Afrika) unaopatikana nchini Tanzania.


Anna Mary alifika kileleni mnamo Novemba 6, 2024, na kucheza Taekwondo kwa takribani sekunde 40 katika kilele cha Stella Point, kilichopo mita 5,756 (futi 18,885) kutoka usawa wa bahari, akiwa na umri wa miaka 13, miezi 8, na siku 24.


Rekodi hiyo imetambuliwa rasmi na Indian Book of Records mnamo Disemba 30, 2024 na kuchapishwa katika jarida la IBR Januari 29, 2025.

Taekwondo ni mchezo wa sanaa za mapigano ulioanzishwa nchini Korea unaojumuisha mbinu za kujilinda kwa kupiga mateke na ngumi.


Safari ya Anna Mary kutwaa rekodi hiyo yenye hadhi ya kidunia inamfanya kuwa moja ya watu wadogo zaidi kuvunja rekodi Mlima Kilimanjaro, Mlima mrefu zaidi barani Afrika, wenye urefu wa takribani mita 5,895 kutoka usawa wa bahari. 


Chapisho la “Indian Book of Record” kuhusu rekodi ya Taekwondo iliyovunjwa Mlima Kilimanjaro litasaidia kutangaza Mlima Kilimanjaro ndani na nje ya mikapa ya Taifa la India kutokana na umaarufu wa jarida hilo. Mlima Kilimanjaro unasifika kuwa Mlima mrefu uliosimama peke yake duniani ukiwa na zaidi ya kanda tano (5) zenye tabia ya hewa tofauti tofauti (“Climatic Zones”).






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI