RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kutokana na kifo cha Mkuu wa Wilaya Mbozi, mkoani Songwe, Esther Mahawe, ambaye amefariki dunia, hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro mapema leo 14, Januari 2025.
Kutokana na kifo hicho, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa wafiwa na kumuelezea kiongozi huyo, kwamba enzi za uhai wake Esther alikuwa Mchapakazi, Msemakweli na mwenye msimamo thabiti.
Aidha, Waziri wa TAMISEMI pia ameweza kutoa taarifa kwa Umma kufuatia Kifo hicho.
0 Comments