Header Ads Widget

MONGELLA AWAPA SIRI MABAROZI KUPATA USHINDI UCHAGUZI MKUU

 

Na Hadija Omary 

Lindi...

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu Naibu Katibu wa chama cha mapinduzi CCM bara bwana John mogella amewataka mabarozi Nchini kudumisha mshikamano ili kuhakikisha  chama hicho kinapata ushindi Katika Uchaguzi huo 

Mongella ametoa wito huo alipokuwa anazungumza Katika mkutano maalumu wa mabarozi wa Jimbo la Mchinga uliofanyika huko tarafa ya Mchinga kijiji cha Mchinga moja Manispaa ya Lindi Mkoani Humo

Amesema Ili kuweza kupata ushindi Katika Uchaguzi huo na chaguzi zinazoendelea ni muhimu kuwa na mshikamano Katika kupanga mikakati ya ushindi kwa pamoja 

Salma Rashid kikwete ni mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi amesema Mkutano huo wa mabarozi wa Jimbo la Mchinga ni mahususi kwa ajili ya kupeana mikakati na mipango ya halmashauri ili kuhakikisha wananchi wanajitokeza kujiandikisha Katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura



Amesema Katika kuhakikisha chama hicho kinashinda kwa kishindo ni muhimu kuwepo na Wapiga Kura wa kutosha ambao watapiga Kura na kukichagua chama hicho siku ya uchaguzi utakapofika 

Amesema zoezi hilo la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa Mkoa wa Lindi litaanza January 28 na kutamatika February 3 mwaka huu.


Baadhi ya mabarozi walioudhurika Katika mkutano wamesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahamasisha wanachama kujiandikisha muda utakapofika




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI