Na Mwandishi Wetu, Momba.
JESHI la polisi Mkoai Songwe linamshikilia, Junge Jilatu(28) Mkazi wa Kijiji cha Namsinde, kata ya Mkulwe, Wilayani Momba kwa tuhuma za mauaji ya watoto wake wawili.
Pia jeshi hilo linawashikilia watu wengine wawili wote wakazi wa kijiji hicho wakihusishwa na tukio hilo la Mauaji.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga, leo Januari 13,2025 imesema tukio Hilo limetokea Januari 11,2025 majira ya saa 2:20 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa.
Kamanda Senga amesema mtuhumiwa aliwakaba watoto hao wakiwa wamelala na kuwakatana kitu chenye ncha kali shingoni kisha mmoja ya watoto hao kumtupa kwenye mtaro wa maji kandokando ya barabara inayokwenda Namsinde.
Amewataja watoto waiouwawa kuwa ni Lwambo Charles(3) na Kamba Charles mwenye umri wa miezi miwili.
"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo baada ya baba wa watoto hao kumtuhumu mtuhumiwa ambaye ni mke wake kuwa amezaa na ndugu wa karibu wa familia take na uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Senga.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja majina ya watu wengine wawili ambao imedai kuwasgikilua ikiwahusisha na tukio hilo la kikatili.
0 Comments