Header Ads Widget

WATU WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KATIBU WA CCM KILOLO

Na MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA

WATU watatu wamekamatwa na jeshi la  polisi mkoani Iringa  kwa tuhuma za mauaji yaaliyekuwa  katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM ) wilaya ya kilolo mkoani Iringa Christina Kibiki  aliyeuawa nyumbani kwake baada ya kuvamiwa  na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Novemba 13 mwaka huu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi alisema kuwa jeshi la polisi limeendelea na msako ambapo waliwakamata watu mbalimbali waliohojiwa na kuachiwa huku watuhumiwa watatu wa wakiendelea kushikiliwa.

SACP Bukumbi lisema kuwa bado wanaendelea na msako  na kuna baadhi ya watu ambao wanatarajia kuwakamata kwa mahojiano na pindi watakapojiridhisha katika upelelezi  wao watawafikisha mahakamani kwa hatua zinazofuata.

Aidha  Bukumbi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kuwafichua waharifu mbali mbali kwani   ushirikiano wa jeshi la polisi na wananchi utasaidia kupunguza uhalifu kwa kuwa wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano katika kufichua vitendo vya uharifu.

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani Iringa linawasaka askari  namba F. 4987 sajent rogas wakituo cha polisi  Ipogolo na askari wa jeshi la akiba Mgambo Thomas Mkembela kwa tuhuma za kumuua Nashon Kiyeyeu (23) mkazi wa nyamhanga kata ya kitwiru Manispaa ya iringa.

Kamanda  Bukumbi alisema kuwa mauaji hayo yametokea Disemba 14 mwaka huu ambapo sajent Rojas kwa kushirikiana na mgambo walimkamata mtuhumiwa Nashon Kiyeyeu kwa tuhuma za kuiba simu na kudaiwa kumpiga mtuhuniwa huyu hadi kupoteza fahamu .
Alisema kuwa sajent Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye hakumtaja jina kuwa anamtuhumu Nashon Kiyeyeu amemuibia simu, ndipo sajent Rogers kwa kushirikiana na mgambo Thomas Mkembela walimkamata mtuhumiwa .

Kamanda SACP Allan Bukumbi alisema baada ya kumkamata wanadaiwa kumpiga mtuhumiwa huyo walipoona amepoteza fahamu wakampeleka hospitali binafsi na baadaye wakampeleka Hospital ya Rufaa ya Iringa na ikabainika mtuhumiwa huyo amefariki dunia.

Alisema kuwa baada ya kuona mtuhumiwa huyo amefariki kutokana na kipigo walitoweka wasikojulikana ambapo jeshi la polisi mkoa wa Iringa linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao pamoja na kusambaza taarifa mikoa mbalimbali.

SACP Allan Bukumbi ametoa wito mtu yeyote atakayemuona sajent Rogers na Mgambo Thomas Mkembela watoe taarifa wakamatwe na hatua zingine za kisheria zifuate.

SACP Bukumbi aliesema kuwa jeshi la polisi mkoani Iringa halita sita kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote ambaye ataonekana kuvunja sheria.

Kwa upande wake baba mzazi wa kijana aliyeuawa mikononi wa asikari huyo Lusia Kiyeyeu alisema alipata taarifa kutoka kwa dada yake alikokuwa anafanya kazi kuwa Nashon amekamatwa na polisi anaelekea kituo cha polisi Ipogolo.
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alifuatilia kituoni hapo hakumkuta kijana wake wala askari aliemkamata na baada ya kuuliza ikaonekana hakufunguliwa jarada kituoni hapo.

Kiyeyeu aliongeza kuwa baadae alifika kituo kikuu cha mkoa wa Iringa lakini pia hakufunguliwa jarada katika kituo hicho.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI