Header Ads Widget

WATU WASIOJULIKANA WANAPANGA NJAMA KUNIUMIZA-LISSU


Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu ambaye pia ni Mgombea Uenyekiti wa Chama hicho, amesema Watu wasiojulikana wanapanga njama za kumuumiza kisha wamsingizie Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambapo amewataka waache kufanya wanalopanga kwakuwa watamchafua zaidi Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda.

Kwenye taarifa yake aliyoitoa leo December 16,2024, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Tundu ameandika yafuatayo "Enyi Watu wabaya mjulikanao kama 'Watu wasiojulikana, nimezisikia njama zenu, mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa Chama, Freeman Mbowe, ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe, ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept '17 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao"

"Ndivyo mavyofanya kila mnapoua Watu wasio na hatia, mnasingizia Watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu, huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani, Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo Bungeni"

"Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda mtamchafua zaidi na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept '17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI