Header Ads Widget

WATU TISA WAFARIKI DUNIA KWA AJALI ROMBO.



ROMBO. 



WATU tisa wamefariki Dunia baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kutoka Tarakea wilayani Rombo kugongana uso kwa uso na basi la Ngasere lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Rombo. 


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mangwalla alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya jioni katika maeneo ya Tarakea. 



Alisema kuwa, katika ajali hiyo watu tisa ambao ni wakiume watano na wakike wanne waliokuwa katika Noah walifariki Dunia papo hapo huku mpaka sasa yupo majeruhi mmoja ambaye amekimbizwa hospitali ya Huruma kwa matibabu. 



Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo Dereva wa Noah alikuwa akilipita gari jingine ndipo alipokutana na basi na Ngasere na kugongana nalo uso kwa uso. 


MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI