Header Ads Widget

SERIKALI INAKUSUDIA KUFANYA UTAFITI WA TATU...




SERIKALI imekusudia kufanya Utafiti wa tatu kubaini hali ya upatikanaji na matumizi ya nishati kwa Tanzania bara  kwa mwaka 2024 kwa kuhusisha Kaya za Mijini na vijijini ambapo Jumla ya wadadisi 110 wameandaliwa kufanya Utafiti huo kwenye Kaya 10,500


Utafiti huo unakusudia kufanywa na  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Nishati vijijini REA katika kipindi cha siku 30.


Akizungumza mjini Morogoro na wadadisi wanaoandaliwa kwa zoezi hilo,Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa alisema Utafiti huo ni muhimu sana  kwa maendeleo ya nchi hasa katika kutekeleza Maendeleo endelevu ya dunia ya mwaka 2030, Dira ya Taifa ya 2025 inayomalizika na ambayo haiwezi kumalizika bila kuwa na taarifa sahihi, na Dora ya Taifa ijayo ya mwaka 2025 hadi 2050.


 "Mpango wa Serikali ni kuhakikisha ndani ya miaka kumi ijayo, yaani kuanIa 2024 hadi 2034 Watanzania wanakuwa wanatuma Nishati Safi kupikia, na  ndio maana mwaka Jana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan alizindua mpango wa Nishati Safi kupikia, sasa kama nchi hatuwezi kwenda ilimradi tumekwenda bila kuwa na malengo na malengo yatafikiwa kwa kuwa na Utafiti utakaobaoni Kile kilichopp, wananchi Wana mahitaji gani nk, Utafiti ndio utaleta majawabu ya kila.kitu, mahitaji na nini vifanyike"Alisema Mtakwimu Mkuu wa Serikali.


Akasema katika Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, Takwimu za matumizi ya Nishati kwa wananchi zilikuwa NI asilimia moja Tu  tena kwa wananchi hasa wanaoishi kwenye majiji kama ya Dar, Mbeya, Mwanza, Tanga na kwingineko, Takwimu ambazo zilikuwa NI za nchini mno ikilinganishwa na Sensa ya mwaka 2002 ambapo matumizi yaliendelea kukua kufikia asilimia 16 ya Kaya zote, maendeleo ambayo ni makubwa..


"Na sasa Takwimu hizi mpya baada ya Utafiti tunategemea zitakuja mabadiliko mengine makubwa zaidi, Takwimu NI muhimu kufikia maendeleo yeyote ndio.maana hata Rais wa Kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere katika.miaka 63 iliyopita wakati nchi ikipata Uhuru, aliamini katika umuhimu wa takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi, na ndivyo alivyowaridhisha Marais waliomfuata"Alisema Dkt Chuwa.


Akasema Mwalimu Nyerere alisema ili nchi iendelee inahitaji mambo makubwa matatu, watu, Siasa Safi na Uongozi Bora, na alisema hangeweza kupeleka huduma za kijamii katika maeneo ya watu waliotawanyika tawanyika ndio maana akaja na wazo la kuanzisha vijiji vya ujamaa ili kufahamu idadi ya watu katika maeneo hayo na kuwafikishia huduma.



Naye Kamishna wa Sensa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Anne Makinda alisema jjukumu la uzalishaji na usambazaji wa Takwimu rasmi ni zoezi jumuishi na sio  jukumu la Serikali Peke yake kama.ambavyo baadhi ya watu wanafikiri.


Akawasisitiza watendaji wa Kata, Wenyeviti wamitaa na vijiji na watendaji wengine wote kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wasimamizi wa utafiti huo.kwa kutoa na kupata taarifa sahihi kwa maswali yatakayoulizwa wakati wa Utafiti.


"Niwahakikishie wananchi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura ya 351, taarifa zote zitakazokusanywa nitakuwa ni Siri na zitatunzwa kwa usiri mkubwa na kutumika kwa shughuli za kitakwimu Tu."Aliwaondoa hofu wananchi Mhe Makinda kuhusu usiri katika Yale watalayoulizwa na kujibu kwa wadadisi.


Kuhusu sekta ya Nishati, Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,imeendelea kutambua umuhimu wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchi kwa kutekeleza mipango na program mbalimbali za maendeleo kwa kuhakikisha umeme wa kutosha unakuwepo na kusaidia kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama Reli ya kisasa ya SGR ña kuzidi kuvutia wawekezaji katika uzalishaji wa bidhaa na huduma na kuimarisha uchumi na Maisha ya wananchi.


Akasema ali ya upatikanaji wa Nishati Tanzania bara kwa mwaka 2019 uliofanywa na NBS kwa kushirikiana na REA ilionesha upatikanaji wa Nishati ulikuwa ni kwa asiilimia78.5, mjini ulikuwa asilimia 99.6 na vijijini asilimia 69.6 Sawa na ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka 2016 ambapo kwa vijijini ilikuwa ni asilimia 49.3 Sawa na ongezeko la asilimia 21"Alisema Makinda.



Akasema Utekelezaji wa mpango kabambe wa kupeleka Umeme Vijijini umewezesha jumla ya vijiji 12,240 Kati ya vijiji 12,318 vya Tanzania bara  kufikiwa na umeme hadi kufikia Novemba mwaka huu na umeme wa bei nafuu na wa kuaminika na nguvu zaidi nimeelekezwa kwenye vitongoji.


Kamishna huyo wa Sensa akasema usambazaji wa umeme vijijini utaharakisha Utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya Nishati Safi na salama ya kupikia ambao umelenga ifikapo 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatuma Nishati hiyo na kwenda sambamba na jitihada za Serikali za kupambana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya Nishati za kupikia zitokanazi na kuni na Mkaa.


Naye Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka NBS Be Daniel Masolwa Alisema Utafiti huo utafanyika Ndani ya siku 30 hivyo kuomba wananchi watakaofikiwa kutoa ushirikiano.


Mwakilishi WA REA mhandisi Salma Bakari alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila.mtanzania anafikiwa na umeme wa uhakika, ndio maana wako kwenye malengo ya kufikisha umeme katika viijiji vyote kwa .mwaka huu na baadaye kwa vtongoji vyote nchini.


Akaasema huu ni Utafiti wa tatu kufanyika kwa kushirikiana na NBS ukitarajiwa kuleta matokeo chanya baada ya kufahamu uhalisia wa mahitaji  ya upatikanaji wa Nishati na matumizi yake na kuyafanyia kazi.


Mwakilishi huyo wa REA Alisema yangu uanzishwa kwa REA  mwaka 2007  wameweza kutekeleza miradi 428  ilipofika Juni mwaka huu ikiwemo inayohusika na gridi ya Taifa na nje ya gridi Taifa na kwamba wameendelea kupambana  kufikisha nishati Safi na Bora vijijini na kuhimiza wadadisi kujali shughuli hiyo iliyo mbele ya Utafiti kwani matokeo yake yanategemewa sana katika.maendeleo ya nchi na mahusiano na wafadhili mbalimbali.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI