Header Ads Widget

MBARONI KWA KUKUTWA NA MALI ZA WIZI

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imemkamata mtu mmoja mkazi wa Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma akiwa na mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa zimepatikana kwa njia ya uhalifu.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Filemon Makungu akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kigoma alisema kuwa mtu huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita na polisi waliokuwa doria walipomshuku kuwa na mali ambazo zinaaminika ni za wizi.

Kamanda Makungu amekataa kutaja jina la mtuhumiwa huyo akieleza kuwa kwa sasa jina linahifadhiwa wakati uchunguzi Zaidi kuhusu tukio hilo na kama kuna watuhumiwa wengine na mtandao ambao alikuwa akishrikiana nao.

Alitaja mali ambazo zilikamatwa kuwa ni Pamoja na TV nne, majiko sita ya gesi ya kupikia, stop koki nne za mabomba ya maji na nyaya za aina mbalimbali za umeme ambazo hakuwa na majibu sahihi ya umiliki wa mali hizo.

Sambamba na huyo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa polisi wilayani Kasulu walimtia mbaroni mtu mmoja wilayani humo kwa tuhuma za kukutwa na pikipiki moja aina ya Kinglion ambayo hakuwa na nyaraka za umiliki wa pikipiki hiyo.

Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amehifadhiwa katika kituo cha polisi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo upelelezi wa shauri hilo unaendelea ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI