Header Ads Widget

CCM YAWATAKA WAUMINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI



Na Matukio Daima App, Maswa.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu,  Shemsa Mohammed amewataka waumini wa Dini mbalimbali kuonyesha Umuhimu wa Mshikamano na Ushirikiano kati ya Taasisi za Dini na Serikali ili kuleta maendeleo katika jamii.

Mwenyekiti Shemsa ameyasema hayo leo kwenye harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Maswa (KKKT), iliyolenga la kuchangia Maendeleo ya kanisa hilo. 


Akizungumza wakati wa harambee hiyo, Shemsa amesema kuwa CCM, kama Chama Tawala, kinaunga mkono juhudi za kijamii zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi na kudumisha amani na mshikamano nchini.

"Mshikamano wetu ndiyo Msingi wa Maendeleo... Tukidumisha upendo na kushirikiana, kila jambo linawezekana, amesema Mwenyekiti Shemsa.

Aidha, Shemsa amewahimiza wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu kuendelea kushirikiana katika miradi ya maendeleo, huku akitoa wito wa kudumisha Amani, Mshikamano, na Maadili mema.


Harambee hiyo ililenga kuchangia ujenzi wa hosteli na uzio wa kanisani, hatua muhimu katika kuboresha miundombinu na usalama wa kanisa.

Katika tukio hilo, Mwenyekiti huyo pamoja na wadau wengine, wamechangia jumla ya shilingi Mil. 15  kati ya shilingi Mil. 33.2  zilizokusanywa kwenye harambee hiyo huku waumini wakimpongeza Shemsa kuwa mfano wa kujitoa kwa dhati katika Kusaidia Taasisi za Dini na jamii kwa ujumla.

Waumini wa KKKT pamoja na viongozi wa kanisa hilo  wametoa shukrani zao za dhati kwa Mwenyekiti huyo juu ya mchango wake mkubwa na kwa kuthamini kazi ya Mungu kupitia kanisa na kwamba Harambee hiyo inatarajiwa kusaidia ukamilishaji miradi ya ujenzi wa hosteli na uzio, hatua ambayo itaongeza thamani na huduma za kijamii kupitia kanisa hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI