Header Ads Widget

AJALI YA MOTO, WATU NANE WALAZWA, CHANZO DUMU LA PETROL

 

Na Moses Ng'wat, Mbozi.


WATU nane wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyopo Mjini Vwawa, baada ya kujeruhiwa katika ajali ya moto baada ya duka la kuhifadhi na kuuza vinywaji vya jumla na rejareja (Depo) kuwaka moto unaodaiwa kusababishwa na mafuta ya petrol yaliyohifadhiwa ndani.


Ajali hiyo ilitokea Disemba 19, 2024 katika kijiji cha Ihowa, Kata ya Ruanda, Wilayani Mbozi, kwenye nyumba ambayo iliyokuwa ikitumika pia kama duka la kuuza vinywaji vya jumla na rejareja (depo). 



Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihowa, Spidi Mbembela, amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa, majeruhi wengi wa ajali hiyo ni wale waliofika eneo la tukio kwa lengo la kuokoa baada ya moto kulipuka ndani ya duka hilo la kuhifadhi na kuuza vinywaji (Depo).


"Majeruhi wengi ni wanaume waliokuwa jirani na eneo la tukio wakiangalia mechi ya mpira wa miguu iliyokuwa ikiendelea (Yanga dhidi ya Mashujaa) ambapo walifika kwa ajili ya kuoka na kujikuta wakijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali" alisema Mbembela. 


Alisema chanzo cha ajali hiyo ni kulipuka kwa dumu la mafuta ya Petroli lilikuwa limehifadhiwa ndani wakati mama mwenye nyumba hiyo, Rose Patrick, akiwa anaanda chakula ndani ya duka hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari, mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi, Dkt. John Mwanyingili, alikiri kupokea majeruhi hao nane  ambapo walifanyiwa uchunguzi wa awali.


Alisema majeruhi hao walifikishwa Hospitalini hapo majira ya saa 12 za jioni ya Disemba 19, 2024 na kupokelewa katika kitengo cha dharura ambapo walifanyiwa uchunguzi wa awali na kuanza kupatiwa matibabu.


Aliwataja majeruhi hao, kuwa ni Rose ambaye ndiye Mama mwenye nyumba kulikotokea ajali hiyo ya moto,pamoja na Isambi Mwene(34),Maneno Jullius (49),Fadhiri Festo(32),Lewis Patrick(19), Frank Msyan(40) na Matokeo Islam(51).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI