Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka wanachana na mashabiki wa chama hicho kutosusia kupiga kura katika maeneo ambayo Chama hicho hakina wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao wanagombea.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa Kigoma kwenye mkutano uliofanyika vuwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma na badala yake ametaka wanachama wa chama hicho kupiga kura za hapana ambako wagombea wa CCM wanagombea peke yao.
Sambamba na hilo Zitto alisema kuwa maeneo ambayo ACT Wazaledo imesimamisha wagombea wanachama hao wanapaswa kupiga kura kuwachagua wagombea wa ACT ili kurudisha mikononi mwa chama hicho kamati za maendeleo za kata kwa kuwa na wajumbe wengi kutoka kwenye vijiji.
Hatutaki msusie kupiga kura kama hakuna mgombea wa ACT pigeni kura ya hapana.
Huu ni uchaguzi wa hasira kwa kilichofanyika mwaka 2020 hivyo mpigie mgombea wa ACT kama hamna pigeni kura za hapana uchaguzi utarudiwa.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amewaonya wasimamizi wa uchaguzi na watendaji wa serikali kutojiingiza kwenye mpango wa kuingiza kura za bandia kwenye books la kupigia kura kwani dua ya ngamia iliyosomwa kwa kuwatumia wazee wa mji wa Kigoma Ujiji ina madhara makubwa kama hawatakubali kusikiliza ushauri huo.
Zitto alihitimisha kampeni hizo huku kukiwa na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha lakini viongozi, wanachama na washabiki wa chama hicho waliendelea kuwepo eneo la mkutano kumsikiliza kiongozi huyo.
0 Comments