Vijana wametakiwa kuacha kulalamika kuhusu utendaji kazi wa viongozi wao na badala yake wawe mfano kwa kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi mbali mbali ambazo ndizo zenye maamuzi ya kuwaweka madarakani viongozi wanaowahitaji.
Rai hiyo imetolewa na mwanahabari Shalom Robert wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kuwahamasisha vijana na jamii kwa ujumla kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwapigia kura viongozi waadilifu.
Shalom amesema vijana wengi wamekuwa msitari wa mbele kulalamika kuhusu utendaji kazi wa baadhi ya viongozi kwenye maeneo yao lakini wamekuwa hawashiriki kwenye chaguzi na kupelekea baadhi ya viongozi wanaochaguliwa kukosa sifa
‘vijana wengi tumekuwa na malalamiko sana juu ya baadhi ya viognozi kuwa hawafanyi kazi lakini ukiangalia hao hao vijana hawajitokezi kwenye chaguzi kuwapigia kura watu wanaowataka na kinachosalia ni lawama’amesema shalom.Aidha amempobgeza Rais Dkt.Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuwataka vijana kuendelea kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii sanjari na kupinga masuala ya uvunjifu wa amani kwa taifa la Tanzania
0 Comments