Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida wametoa onyo watu,vyama na baadhi vikundi ambavyo vimekuwa na tabia ya kutweza na kudhihaki kazi kubwa za maendeleo zinazofanywa na serikali hawatavumiliwa watashughulikiwa.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Singida, Dk.Denis Nyiraha, akizungumza leo (Novemba 13, 2024) na waandishi wa habari kuelezea maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita, amesema hakuna sababu kwa mtu au chama kubeza mambo yanayofanywa na serikali ya CCM.
"Nataka tuwatumie salama kama walikuwa wanafanya haya mambo kipindi cha nyuma waache,kama walikuwa wanafikiri Rais Samia Suluhu Hassan hana vijana ambao wapo nyuma yake sasa tunataka tuwaambie waache vijana tupo tumevumilia vya kutosha," amesema.
Nyiraha amesema vijana wa CCM hawatakuwa tayari kunyamaza kuona kuna genge la mtu yeyote awe ndani ya chama au nje akibainika anabeza kazi zinazofanywa na serikali atashughulikiwa ipasavyo.
"Atakayedhihaki kazi kubwa na weledi wa Rais Samia Suluhu Hassan atakayefanya hivyo sisi vijana wa CCM tutamshughulikia ipasavyo," amesema Nyiraha.
Amesema katika utawala wa rais wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere alipigana mambo makuu matatu ambayo ni kuondoa umaskini,ujinga na maradhi mambo ambayo rais Samia ameendeleza kazi hiyo kwa kuweka misingi ya uimara.
Nyiraha alitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika sekta ya elimu ni ujenzi wa Shule za Msingi na Sekondari zipatazo 3331 na madarasa zaidi ya 21,000 nchi nzima.
Amesema kutokana kuboreshwa kwa sekta ya elimu hata kiwango cha uandikishaji wanafunzi wa madarasa ya awali kimeongezeka kutoka wanafunzi 1, 292,921 na kufikia 1,679 562 na kwamba kwa Mkoa wa Singida Shule za Msingi 673 na Sekondari 183 zimejengwa.
Katika sekta ya afy kwa Mkoa wa Singida, alisema katika kipindi cha 2020 kulikuwa na maboma ya zahanati 101 lakini hadi kufikia 2024 yapo 116,vituo vya afya vilikuwa 21 lakini sasa vipo 31.
"Kama vijana tunamshukru Rais Samia kwa namna alivyoweka misingi ya kuinua maisha ya wananchi na hivyo vijana wa Singida 2025 hatuna mbadala wa rais zaidi ya Samia Suluhu Hassan," amesema.
0 Comments