NA MATUKIO DAIMA MEDIA
SINTOFAHAMU yaibuka mauaji ya Kinyama ya aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Christina Alex Kibiki (56) kuhusu aina ya Kifo chake wajukuu Wadai kabla ya kuuwawa wauaji walimbaka sebuleni Kisha kumuingiza ndani kumuua na kitu chenye ncha Kali.
Asifiwe Kibiki ni shuhuda wa mauaji hayo alisema kuwa wauaji hao walikuwa zaidi ya watatu mmoja aligonga mlango kuwa anashinda na bibi yao.
"Baada ya kugonga mlango walimuuliza bibi na wakati bibi akitoka nje kwenda kumsikiliza ghafla walimgeuzia kibao na kuanza kumshambulia na kumvutia ndani huku dada yangu alipojaribu kumsaidia alipigwa na kuanguka chini "
Alisema baada ya hapo dadake kuanguka chini mtu huyo asiyejulikana alimvutia ndani bibi yao na kuanza kumbaka na wakati huo Wao walikimbia nje kupiga kelele kuomba msaada .
Kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na amesema silaha ya kienyeji mfukoni mfano wa bastora hali iliyowafanya kuogopa zaidi .
"Huyu mtu mmoja aliyekuwa akimbaka bibi aliingia ndani Pekee yake ila nje Wenzake wawili walikuwa wakiimarisha Ulinzi mmoja alikuwa akinywa soda na mwingine akitazama watu ila sijui kama baadae wote Waliingia ndani "
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumfanyia ukatili huo sebuleni baada ya hapo walimvutia chumbani kwake na kuanza kumchoma na vitu vyenye ncha Kali Kisha kumtupa kwenye box lililokuwa chumbani kwake .
Shuhuda huyo alimweleza mwandishi wa Matukio Daima media aliyefika Kitika kitongoji Cha Banawano, kijiji cha Ugwachanya, kata ya Mseke, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupata undani wa tukio hilo lililotokea majira ya saa 3 usiku wa Novemba 12 mwaka huu.
Tukio hilo limeacha simanzi kubwa kwa familia, majirani, na viongozi wa chama.
Kwa mujibu wa Asifiwe Kibiki, mjukuu wa marehemu, Christina alivamiwa na kijana ambaye hakutambulika mara moja.
.
Asifiwe alieleza zaidi kuwa mvamizi huyo aliingia ndani ya nyumba kwa ghafla na kufanya unyama huo, kisha kumwacha bibi yake akiwa hoi .
"Baada ya shambulio, tulisikia mlipuko kama bomu, na majirani walikusanyika kwa msaada lakini watuhumiwa walikuwa tayari wametoroka," aliongeza.
Festo Mwangamila, Mwenyekiti wa kitongoji cha Banawano, alisema alipofika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu, aliwakuta watuhumiwa wameshatoweka. "Tukio hili ni la kwanza kutokea katika kitongoji chetu na limeleta hofu kubwa," alisema Mwangamila.
Laula Kilienyi, Diwani wa Viti Maalumu katika tarafa ya Mlowe, alimzungumzia marehemu Christina Kibiki kama kiongozi shupavu, mchangamfu, na mpenda watu.
"Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii na uongozi bora," alisema Diwani Kilienyi kwa huzuni.
Shakila Kiwanga, Diwani wa kata ya Kalenga, alielezea jinsi alivyopokea taarifa za tukio hilo saa tano usiku kutoka kwa mtoto wa marehemu. Alifuatilia kwa haraka hadi hospitali ya Tosa Maganga, ambako alikuta marehemu akiwa hoi.
"Lakini baada ya muda mfupi, tulipata taarifa za kifo chake, jambo lililotuuma sana," aliongeza Kiwanga.
Wakati Majukuu wa marehemu huyo akidai bibi yake alibakwa kabla ya Kifo chake Dkt. Thomas Malongo, Mkurugenzi wa Tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tosa Maganga, alisema kuwa walimpokea Christina Kibiki akiwa hajitambui, huku akiwa na majeraha mengi mwilini na kuvuja damu puani na masikioni.
Hata hivyo alisema marehemu aliuwawa kutokana na majeraha ya vitu vyenye ncha Kali Mawili na kuwa hawawajaona dalili za kubakwa .
"Madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake kwa kuzuia damu kuvuja zaidi, lakini kwa bahati mbaya alifariki baada ya saa moja na nusu," alisema Dkt. Malongo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini wahusika.
"Marehemu alipigwa risasi kifuani na kitu kizito kichwani, na watuhumiwa walitoroka bila kuchukua kitu chochote nyumbani kwa marehemu," alisema Kamanda Bukumbi.
Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu hao ili kuhakikisha haki inatendeka.
Tukio hili limetikisa wakazi wa Wilaya ya Kilolo, wakiwacha wakihitaji majibu na haki kwa kifo cha kiongozi wao mpendwa.
Mwisho
MATUKIO DAIMA MEDIA NI KATI YA VYOMBO VIWILI VYA MITANDAONI TANZANIA VILIVYO TEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS.
JINSI YA KUPIGA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA
Ingia katika tovuti ya www.samiaawards.tz
1. Nenda sehemu iliyoandikwa “Piga Kura”
2. Bonyeza neno lililoandikwa NEXT
3. Utaona Makundi ya tuzo, bofya lililoandikwa TUZO KWA VYOMBO VYA HABARI kisha libonyeze hapo
4. Utaona sehemu imeandikwa "VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI" kisha ingia hapo
5. Baada ya hapo utaona jina MATUKIO DAIMA Namba ya Mshiriki NNI 24005006 Kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa PIGA KURA
Ukikamilisha hatua hiyo, utakuwa umepigia chagua *MATUKIO DAIMA*
Asante sana kwa kura yako
KUPIGA KURA KWA SIMU YA KAWAIDA
1:Ingia Uwanja wa Ujumbe
2:andika neno Kura Kisha acha nafasi weka namba 24005006
3:Tuma kwa Namba 15200
HAKIKA UNA SALIO LA KAWAIDA SHILINGI 100 TU SIO KIFURUSHI
HAPO UTAKUWA UMEPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA
🙏 AHSANTE SANA KWA KURA YAKO MAANA KURA YAKO NI USHINDI WETU MATUKIO DAIMA MEDIA NI YETU SOTE MUNGU MWEMA AKUBARIKI KWA KURA YAKO YA THAMANI
0 Comments