Header Ads Widget

TCB YATOA VIFAA VYA 17.5 MILIONI 'KUBUSTI' MICHEZO SONGWE

 


Na Moses Ng"wat, Songwe.

BENKI ya  Biashara Tanzania (TCB) imeungana na serikali ya  Mkoa wa Songwe katika kuinua michezo kwa kutoa msaada wa vifaa vya vyenye thamani ya shilingi 17.5 milioni kwa ajili ya shule za msingi, sekondari na vitalu vya kulea na kukuza vipaji  vilivyopo mkoani hapa. 


Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, kupitia hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa,

Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanjelwa, Mkoani Mbeya, Simon Mlelwa, aliyemwakilisha Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, alisema lengo ni kutimiza azma ya serikali ya  Mkoa ya kuhakikisha michezo inafanyika katika mazingira mazuri.


 ikiwemo, kutatua changamoto ya vifaa vya  michezo mashuleni.


"Sisi kama Benki ya Biashara Tanzania kwa niaba ya Mtendaji Mkuu tunajivunia kushirikiana na jamii yetu kuhakikisha tunatatua changamoto hasa katika sekta ya michezo ili jamii iendelee kuishi katika mazingira mazuri" Alisema Mlelwa kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TCB.


Aliongeza kuwa, TCB imekuwa ikirejesha kwa jamii kupitia maeneo makuu matatu ambayo ni sekta ya Elimu, Afya na Ustawi wa jamii.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Chongolo akipokea vifaa hivyo ambavyo ni Jezi na Mipira, aliipongeza menejimenti ya TCB kwa msaada huo ambao lengo lake ni kuinua na kukuza michezo Mkoani hapo.


"Tunashukuru kwa msaada huu, wiki iliyopita nilikutana na viongozi wa soka wa Mkoa na tukazungumza kwa kirefu kuhusu maendeleo ya michezo kuona namna michezo inakuwa sehemu ya maisha yetu... halafu ghafla mmekuja kutuunga mkono  mkiwa mmejipanga na kutupatia vifaa hivi, hivo narejesha shukurani na mzifikishe kwa mtendaji Mkuu" Alishukuru Chongolo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI