Header Ads Widget

SERIKALI KIGOMA YAAHIDI KUWAUNGA MKONO WABUNIFU CHIPUKIZI

 

Wanafunzi kutoka shule mvalimbali za sekondari mkoani Kugoma waliohuduuria maadhimisho hayo
Katibu wa itikadi,siasa na uenezi CCM mkoa Kigoma Deogratius Nsokolo

Mbunifu wa magari, Sanaa na Mwandishi wa habari Alli Masoud Maarufu Masudi Kipanya akizungumza katika maadhimisho hayo


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SERIKALI mkoani Kigoma imeahidi kuwaunga mkono na kuwaendeleza wanasayansi chipikuzi ili waweze kufanya vizuri na kazi zao zilete matunda katika matumizi ya kawaida ya shughuli za kibinadamu.

 

Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Sayansi yaliyofanyika kwenye manispaa ya Kigoma Ujiji yaliyoambataa na maonyesho ya kazi bunifu za sayansi kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari za manispaa ya Kigoma Ujiji.

 

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa wilaya Kigoma, Mganwa Nzota alisema kuwa kutokana na kazi bunifu za wanafunzi hao zilizoonyeshwa wamevutiwa na kuweka ahadi ya kuwatafutia wabuni hao namna ya kuunganisha bunifu hizo katika karakana na wabunifu wakubwa ili kuinua vipaji vya wabunifu hao chipukizi.

 

Naye Mbunifu wa magari na Mwandishi wa Habari, Alli Masoud maarufu kama Masudi Kipanya akizungumza katika maadhimisho hayo alisema kuwa wanasayansi na wabunifu chipukizi waungwe mkono kwa kazi zao kupelekwa kwenye karakana kubwa ili waweze kufanya mambo makubwa kulinga na mawazo yao ya ubunifu waliyofanya.

 


Kwa upande wake Katibu wa idara ya itikadi na Uenezi  CCM mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo amezitaka mamlaka za serikali katika halmashauri na taasisi mbalimbali zinazosimamia masuala ya ufumbuzi na ubunifu ikiwemo vyuo vya VETA kuipa umuhimu siku ya sayansi hasa maonyesho ya wabunifu chipukizi waweze kuwaendeleza na kuinua vipaji vyao akikemea mamlaka hizo kukimbia kuhudhuria maadhimisho hayo.

Awali Mratibu wa maonyesho hayo Genoveva Mtiti, alisema kuwa wamegundua kuwepo kwa vipaji mbalimbali kwa wanafunzi hivyo wameona ashiriki kusaidia maandalizi na kuwezesha wanafunzi hao kuonyesha kazi zao na kutafuta namna ya kuwapata watu ambao wataendeleza hizo bunifu zilizofaanyika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI