NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameendelea na kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa mitaa katika manispaa ya Moshi ambapo leo alikuwa katika kata ya Bondeni.
Mbunge huyo ambaye aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Priscus Tarimo, Diwani wa kata hiyo na Diwani wa viti maalum, Aisha Gogo na viongozi mbalimbali wa chama.
Alisema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa dhati kuwajali wananchi wa kata hiyo ambapo amepeleka fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Ninyi ni mashahidi tulipata tatizo la kuunguliwa na soko la Mbuyuni lakini Rais kwa kutambua umuhimu wa soko lile ameleta fedha kuhakikisha linajengwa kwa kisasa huu ni upendo mkubwa sisi wanabondeni na manispaa na mkoa kwa ujumla" Alisema Mbunge Zuena.
Na kuongeza "haya yote aliyofanya Rais hataki kulipwa fadhili kwa kupewa kitenga hapana bali sisi wananchi tunawajibu wa kumlipa kwa kuwapa kura wagombea wanaotokana na chama chake cha CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu".
Mbunge huyo alidai kuwa, kwa sasa wananchi wote wa manispaa ya Moshi wameamua kwa kauli moja kuzima zote na kuwasha kijana kwa kuwachagua wagombea wanaotokana na CCM.
Katika kata hiyo ya Bondeni inayo mitaa miwili ambao ni mtaa wa Mbuyuni mgombea wake akiwa, Abdalah Kideko na mtaa wa Sokoni mgombea wake akiwa ni Muki Jama.
Mwisho.
0 Comments