Na Hadija Omary
Lindi....Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi Mama Salma Rashid Kikwete amewaongoza wananchi wa Jimbo hilo kushiriki zoezi la upigaji wa Kura kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Mama Salma ameshiriki zoezi hilo Katika kituo cha kupiga Kura cha Makasini kijiji cha Ruvu Kata ya Mchinga Manispaa ya Lindi.
Akizungumza mara baada ya kupiga Kura Mama Salma Kikwete amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza Katika vituo vya kupigia Kura ili kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia.
Kwa upande wa Msimamizi wa Uchaguzi wa kituo hicho cha makasini Joseph Jeremiah ameeleza hatua za awali kwa wanaofika kupiga kura kabla ya kushiriki kupiga Kura huku baadhi ya wananchi wakieleza namna ya zoezi hilo linavyoendelea.
0 Comments