Header Ads Widget

MADIWANI MBOZI NA MKAKATI WA KUJENGA SHULE 10 ZA KIDATO CHA SITA KABLA YA KUMALIZA MUDA WAO.

 

Na Moses Ng'wat, Mbozi

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbozi imepokea kiasi cha shilingi bilioni 4.7 kutoka serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Kanda ya wavulana, ikiwa ni mkakati mahususi wa kuzuia wimbi kubwa lililoibuka katika Halmshauri hiyo la wanafunzi  wa wavulana kukatisha masomo ukilinganisha na wanafunzi wa kike.

Hayo yamebainishwa Novemba 7, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Doroth Mwandila, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo katika kikao cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha 2024/25 cha baraza hilo, kilichofanyika katika ukumbi wa polisi, Mjini Vwawa.

Mwandila ameaema shule hiyo ya Kanda ya wavulana itakayojengwa katika kata ya Ukwile, ikiwa ni sehemu ya  mkakati wa 

Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mbozi kuwa na shule 10 za kidato cha sita ifikapo mwaka 2025.

Katika majibu ya ziada, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, George Musyani,  amesema kuwa mpaka sasa Halmashauri hiyo ina jumla ya shule nne za kidato cha sita, huku mpango uliopo ni kuongeza shule zingine sita zenye kidato cha tano mpaka kufikia 2025.

Amesema kuwa mkakati huo umelenga kuboresha mazingira ya kujifunza, kuongeza nafasi za masomo, na kutoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kuendelea na elimu ya juu.

"Uanzishwaji wa shule hizi utakuwa na athari chanya katika jamii yetu, ikiwemo kukuza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa elimu ambayo itawafanya wazazi wawe na hamu ya kuwapelela watoto shule" amesema 


Awali akiuliza swali katika baraza hilo, Diwani wa Kata ya Nyimbili, Christopher Ntandala, alitaka kujua sababu za wanafunzi wengi wa kiume katika Halmshauri hiyo wanakatisha masomo ukilinganisha na wakike.

Shule za kidato cha sita zilizopo katika Halmashauri hiyo ni nne ambazo ni shule ya kutwa Vwawa, Simbega, Myovizi na  Mlangali, huku shule nyingine za  kidato cha sita na zinazotarajiwa kufunguliawa ni Itaka, Nanyala, Igamba, Msiya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI