Header Ads Widget

KAULI YA DKT. NCHIMBI MSIBANI KWA BI CHRISTINA /AKEMEA VITENDO VYA KINYAMA

 


Na Matukio Daima media 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka  Watanzania kuungana kukomesha tabia za Kinyama kama ambayo imejitokeza kwa Bi. Christina Kibiki ambaye amefariki kwa kuvamiwa na kupigwa risasi na Watu wasiojulikana Usiku wa Novemba 12, 2024 akiwa nyumbani kwake. 


Hayo ameyazungumza wakati wa mazishi ya Christina Kibiki ambayo yamefanyika leo Novemba 15, 2024 nyumbani kwake Kitongoji cha Banawanu, Kata ya Mseke Wilaya ya Iringa Vijijini ambapo Viongozi mbalimbali wa Serikali, Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Viongozi wa dini na Wananchi wameuhudhuria katika mazishi hayo. 



"Tabia kama hizi ni tabia za kinyama ambazo hazikubaliki katika Taifa, ni tabia ambazo zinapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania tabia kama hizi zinapoanza kuibuka ibuka kwenye Taifa sio tu zinaleta majonzi na huzuni lakini pia zinazaa hofu na mashaka kwa Wananchi" amesema nchimbi. 


Akitoa salamu za Serikal Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amesema kuwa Uchunguzi unaendelea na kuwataka Wananchi kutoa Ushirikiano ili kuwakamata Wahalifu hao na kukomesha matukio ya kikatili katika nchi yetu.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI