Na Moses Ng'wati, Songwe.
KAMATI ya Amani Mkoa wa Songwe imetoa rai kwa wakazi wa Mkoa wa Songwe kujitokeza kwa wingi kama walivyojiandikisha kushiriki kuueachagua viongozi wataokuwa chachu ya maendeleo yao.
Rai hiyo imtolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ya amani Mkoa wa Songwe, Shekhe Hussein Batuza, wakati akizungumza na vyombo habari mbalimbali Mkoa hapa.
Batuza alisema kitendo cha wananchi kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kujiandikisha kunapaswa kwenda sanjari na upigaji kura kura unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Kadhalika, Shekhe Batuza amewataka wananchi kuhakikisha wanalipa kipaombele suala la kulinda amani katika kipindi chote cha mchakato wao unaoshirikisha zoezi la kuwachagua viongozi hao wa serikali za mitaaa.
Vile vile amekemea vikali watu wanaopanga au walipanga kutoa vitisho , ubaguzi wa dini au kabila na kusema vitendo hivyo vikiachwa vinaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake, Mchungaji Rodgers Simkonda ambaye ni katibu wa kamati hiyo alionya juu vitendo vya rushwa na kusema viongozi wanaopatikana kwa rushwa ni batili hata kwa mungu.
0 Comments