Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mlundikano wa Michango na Kero nyingine kwa wakazi wa Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe kumetajwa kumnyanyua Emmanuel Kayombo kwenda kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Serikali za Mitaa kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ili akapambane kukabiliana nayo.
Akizungumza wakati akinadi sera zake katika eneo la Kambarage Getini Mgombea Huyo bwana Kayombo amesema adha inayowakumba wananchi juu ya michango mingi pamoja na changamoto nyingine zimemlazimu kuomba ridhaa ya Uenyekiti wa Serikali za Mitaa ili akawatetee.
Aidha Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati Emmanuel Masonga amesema wananchi ndio wenye maamuzi ya maendeleo wanayoyataka katika kipindi cha miaka mitano Ijayo kwa kuchagua viongozi watakaowasaidia.
Kwa upande wao wakazi wa Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe akiwemo Veronika Mwalongo wanakiri kuwapo kwa michango mingi ambayo imekuwa mwiba mkali katika mtaa wao jambo ambalo linawasukuma kuchukua hatua katika kukabiliana na adha hiyo.
Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinatarajiwa kuhitimishwa Novemba 26 Tayari kwa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Hapo Novemba 27 Mwaka Huu.
0 Comments