Header Ads Widget

TSH. BILIONI NANE KUTUMIA MRADI WA TUAMKE PAMOJA

 



Na Hamida Ramadhan matukio Daima App DODOMA

MENEJA Mradi wa Tuinuke Pamoja wenye lengo la kutatua changamoto za kijinsia zilizopo katika ngazi ya jamii Nestory Mhando amesema kwa kipindi cha miaka mitatu katika mkoa wa Dodoma kiasi cha Sh. bilioni nane kinatarajiwa kutumika kuteleza mradi wa 

Alibainisha hayo jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo wenye lengo la kuleta usawa wa kijinsia katika ngazi ya jamii.

Amesema, fedha za ufadhili wa mradi huo ni kutoka Ubalozi wa Ireland ambapo utatekelezaji wake unafanywa na mashirika mawili ambayo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) pamoja na Aga Khan Foundation (AKF).

Mhando, amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha kupelela rasirimali fedha kwa vikundi ambavyo vipo katika ngazi ya jamii vilivyo jikitaka kupambana na changamoto za usawa wa kijinsia.

“Kwahiyo lengo la mradi ni kuhakikisha usawa wa kijinsia lakini pia kuinua wanawake na katika hilo kuna maeneo makuu matatu ya kwanza ikiwemo kupeleka rasirimali fedha kwa vile vikundi lakini eneo la pili ni kuwajengea uwezo vile vikundi waweze kuwa na taaluma stahiki kwenye utelezaji wa hiyo miradi ambayo wao watakuwa wamebuni.

Aidha ameseeleza eneo jingine ni kuviunganisha vikundi pamoja na mitandao inayohusiana na masuala ya jinsia haki za wanawake watoto lakini pia watu wote kwenye jamii ili mashirika hayo makubwa yaweze kujifunza .

" Lengo kuu pia  vikundi piwa viweze kujifunza kutoka kwa mashirika hayo makubwa halafu sasa ule uzoefu kwa pamoja uweze kutusaidia kuondoa changamoto za kijinsia katika jamii yetu”amesema Mhando

Alisema eneo kubwa jingine ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na majukwaa ya mijadala ambayo yataleta pamoja serikali wadau wa maendeleo wanaharakati vikundi lakini pia wanajamii.

“Majukwa haya yatasaidia kuangalia muktadha mzima wa masuala ya kijinsia, changamoto za kijinsia na mikakati ya utekelezaji lakini pia namna ambavyo sasa tunaingiza masuala ya kisera kwenye mambo ambayo yanahitaji utatuzi wa kisera zaidi”alisisitiza

Kadhalika, alisema mradi huo ni wa miaka mitatu na kwa makubaliano ya utekelezaji ni kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja.

“Kwa huu mwaka wa kwanza kiasi ambacho tunaenda kukitumia ni takribani bilioni mbili ambazo katika hizo fedha asilimia 50 kitaenda moja kwa moja kwenye ile jamii tunayoilenga katika maana ya kwamba hivi vikundi ambavyo vimejikita kwenye masuala ya kijinsia kwasababu ndicho tunachokitaka na tunataka rasirimali nyingi iende huko,”amesema

Vile vile, amesema katika mwaka wa pili na wa tatu wanatarajia kuwa na kiasi kingine ambacho kitakamilisha kiasi hicho cha bilioni nane ambazo zimewekezwa ili kuwa na jamii yenye usawa.

“Jamii inayoishi kwenye usawa ambayo haina vitendo vya ukatili dhidi ya jinsia au dhidi ya mtu yoyote lakini pia jamii ambayo inazingatia usawa, haki nafasi sawa katika nyanja zote za uongozi lakini pia katika umiliki wa rasirimali”amesema

Kwa upamde wake Ofisa habari na mratibu wa mradi huo Monica John kutoka TGNP, alisema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika hayo mawili ili kuwezesha vikundi katika ngazi ya jamii kuwa na harakati za pamoja za kuleta usawa wa kijinsia.

“Mradi huu wa miaka mitatu utatelezwa na TGNP pamoja na Aga Khan Foundation katika kuwezesha vikundi katika ngazi ya jamii kuwa na harakati za pamoja kuleta usawa lakini pia kuviwezesha vikundi hivyo rasirimali fedha”amesema

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI