Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Masoka iliyopo Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Ndakidemi alikabidhi vifaa hivyo Oktoba 7 mwaka huu shuleni hapo akitekeleza ahadi yake aliyoitoa siku ya mahafali Oktoba 5.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Masoka Mwalimu Ahmed Litinji alimshukuru Mbunge na kumwahidi kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukuza vipaji vya mchezo wa mpira hapo shuleni.
Katika tukio jingine, akiwa katika viunga vya ofisi yake, Mbunge Ndakidemi alikabidhi vifaa vya michezo kwa vijana kutoka Kata ya Uru Shimbwe, akiwa anatekeleza ahadi yake ya kuwapatia jezi na mpira alipotembelea na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi.
Mwisho
0 Comments