Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI KATIKA KATA YA URU KUSINI



Na WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameendelea na ziara ya kikazi katika Kata ya Uru Kusini na kukagua miradi ya maendeleo.



Ndakidemi aliambatana na uongozi wa CCM Kata ya Uru Kusini, Diwani wa Kata Wiliad Kitally,  Andrew Mwandu, Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini, wataalamu kutoka MUWSA na wataalamu kutoka katika Kata ya Uru Kusini.



Mbunge alitembelea Shule ya Msingi Kariwa ambapo alijionea uchakavu wa madarasa ambapo Uongozi wa shule ulimwomba awasaidie kupata umeme.

 

Mbunge Ndakidemi alipata wasaa wa kutembelea ujenzi unaoendelea wa ofisi ya Kijiji cha Kariwa na daraja linalounganisha Kijiji cha Kariwa Kati na Kariwa Kusini ambapo fedha za Mfuko wa jimbo shilingi milioni 4,452,100.00 zilipelekwa kufanya ujenzi wa daraja hilo.



Akiwa katika mkutano wa hadhara katika eneo la kwa Change katika kijiji cha Longuo A, Mbunge aliwasilisha ripoti ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka minne tokea waingie madarakani mwezi Novembe 2020. 


Aliwaeleza wananchi kuwa kwa kipindi hicho, Kata ya Uru Kusini ilipatiwa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 2,345,630,944.00 ambapo pia aliwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote. 



Katika mkutano huo, wananchi waliwakilisha changamoto kadhaa ikiwemo ubovu wa barabara ya Mringeni - Mwenge pia kuna mwananchi alilalamika kuwa  kituo cha polisi cha Okaseni  hawawatendei haki, bali huwanyanyasa na suala la gharama za juu kujiunga na mfuko wa bima ya afya na ulevi uliokithiri kwa vijana  viliibuliwa katika mkutano wa Mbunge.



Mbunge walishirikiana na Diwani kujibu kero zote huku kero ambazo hazikuwa na majibu walizichukua na kuwahakikishia wananchi kuwa watazipeleka kwenye mamlaka husika. 



Wakizungumza katika mkutano huo kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Uru Kusini, Fredrick Mbararia na Kaimu Katibu wa CCM  Wilaya, Andrew Mwandu waliwashukuru na kuwapongeza Mbunge na Diwani kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuwaletea wananchi wa Uru Kusuni  miradi mingi ya maendeleo, ukiwemo ule wa Kituo cha Afya ambacho kimeanza kuwapa huduma wananchi. 



NMwandu aliwashauri wananchi wajiandikishe na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu. 


Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI